• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
TUSIJE TUKASAHAU: NLC izilipe fidia familia ambazo ardhi zao zilitwaliwa kwa ajili ya ujenzi wa reli kutoka Mai Mahiu hadi mjini Longonot

TUSIJE TUKASAHAU: NLC izilipe fidia familia ambazo ardhi zao zilitwaliwa kwa ajili ya ujenzi wa reli kutoka Mai Mahiu hadi mjini Longonot

MNAMO Agosti 24, 2020 Tume ya Kitaifa ya Ardhi (NLC) iliahidi kuzilipa fidia familia 800 ambazo ardhi zao zilitwaliwa kwa ajili ya ujenzi wa reli kutoka Mai Mahiu hadi mjini Longonot.

“Kamati maalum imebuniwa kuharakisha shughuli ya ulipaji fidia kwa watu walioathiriwa wakati wa utekelezwaji wa mradi huu,” NLC ikasema kupitia taarifa.

Hii ni baada ya wakazi hao kutishia kuwasilisha kesi kortini kusaka agizo la kushinikiza walipwe jumla ya Sh5 bilioni walizoahidiwa.

Lakini huku mjadala kuhusu athari za hatua ya serikali mpya ya Rais William Ruto kuhamisha shughuli za bandari kutoka Naivasha hadi Mombasa ukishika kasi, imebainika kuwa NLC haikuwa imezilipa familia hizo fidia.

Sasa familia hizo zinaitaka tume hii kutosahau kuwalipa fidia kwani wanahofia kupata hasara kubwa baada ya shughuli za upakuaji mizigo kurejeshwa Mombasa.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wachunguza kisa cha kudhulumiwa kwa mwanafunzi wa...

CHARLES WASONGA: Uamuzi wa Spika Wetang’ula kuhusu mrengo...

T L