• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
TUSIJE TUKASAHAU: Rais alishindwa kabisa kukabili jinamizi la ufisadi nchini

TUSIJE TUKASAHAU: Rais alishindwa kabisa kukabili jinamizi la ufisadi nchini

MNAMO Juni 14, 2018, Rais Uhuru Kenyatta aliamuru kuwa serikali yake ikague hali ya maisha ya watumishi wote wa umma kubaini vyanzo vya mali wanayomiliki.

Akiongea mjini Mombasa alipoongoza rasmi ufunguzi rasmi wa barabara ya pembeni ya Dongo Kundu (maarufu kama Dongo Kundu Bypass), kiongozi huyo alisema shughuli hiyo ingeendeshwa kama sehemu ya mikakati ya kupambana na ufisadi katika sekta ya umma.

“Watumishi wa umma kuanzia mimi na naibu hapa (William Ruto) watatakiwa kuelezea asili ya mali yao. Na wale wote watakaopatikana kuwa walipora mali ya umma watasukumwa gerezani. Hakuna atakayesazwa,” Rais Uhuru akanukuliwa.

Miaka miwili baadaye, mnamo Julai 20, 2020, Rais Kenyatta naye alifichua kuwa serikali yake hupoteza Sh2 bilioni kila siku kwa jinamizi hilo la ufisadi. Hii ni sawa na Sh730 bilioni.

Kiongozi huyo wa taifa anapokamilisha muhula wake wa pili na wa mwisho afisini, Agosti 9, akumbuke alifeli kabisa kupambana na vita dhidi ya ufisadi, hususan, katika sekta ya umma.

  • Tags

You can share this post!

Mivutano sasa yatikisa jahazi la Raila Tharaka

Kumbe wana doa!

T L