• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
TUSIJE TUKASAHAU: Ruto awe na msimamo thabiti kuhusu SGR

TUSIJE TUKASAHAU: Ruto awe na msimamo thabiti kuhusu SGR

MNAMO Jumanne wiki hii, Naibu Rais William Ruto aliahidi kubatilisha baadhi ya sera za Rais Uhuru Kenyatta kuhusu usimamizi wa shughuli za bandari na usafirishaji mizigo kwa reli ya kisasa (SGR).

Akiongea katika makazi yake rasmi mtaani Karen alipompokea Gavana wa Kilifi Amason Kingi ndani ya muungano wa Kenya Kwanza Dkt Ruto alisema akishinda urais, ataondoa shughuli za bandari kavu kutoka Nairobi na Naivasha na kuzirejesha Mombasa “ili kutoa nafasi za kazi kwa Wapwani.”

Lakini Dkt Ruto asije akasahau kuwa mnamo Juni 2020, alikashifu Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ambaye alipinga hatua ya kuhamishwa kwa baadhi ya shughuli za bandari ya Mombasa hadi Naivasha.

Naibu Rais alikana madai kuwa hatua hiyo itawapokonya wakazi nafasi za ajira na kuathiri uchumi wa Pwani kwa ujumla.

Isitoshe, Oktoba 20, 2021 wakati wa sherehe za Mashujaa Dei katika uwanja wa Wang’uru, kaunti ya Kirinyaga, Dkt Ruto alimsifu Rais Kenyatta kutokana miradi ambayo serikali yake imetekeleza.

Mradi wa SGR na kugatuliwa kwa shughuli za bandari miongoni mwa mafanikio ambayo Naibu Rais alitaja.

  • Tags

You can share this post!

‘Muuaji’ De Bruyne aweka Man City pazuri

Makabiliano ya Joho na Kingi yafufuka upya

T L