• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 9:49 AM
TUSIJE TUKASAHAU: Walimu wakuu bado wameorodhesha ada nyingi ambazo wanawataka wazazi walipe

TUSIJE TUKASAHAU: Walimu wakuu bado wameorodhesha ada nyingi ambazo wanawataka wazazi walipe

KUANZIA leo Jumatatu, wanafunzi waliofanya Mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) mwaka 2022, wanaanza kujiunga na kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za upili.

Mwishoni mwa mwaka 2022, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alitoa mwongozo wa karo ambapo Shule za Kitaifa zitahitajika kutoza Sh53,554 kwa mwaka.

Wazazi wenye wanafunzi katika shule za upili za mabweni za ngazi za kimkoa watalipa Sh40,335 kila mwaka.

Lakini Waziri Machogu asije akasahau kuwa walimu wakuu bado wameorodhesha ada nyingi ambazo wanawataka wazazi walipe hali ambayo inawaongezea mzigo wa gharama.

Kwa mfano, kuna shule za upili ambazo zinawatoza wanafunzi wa Kidato cha Nne ada za masomo ya ziada, ada za kununua mabasi ya shule, ada za michezo miongoni mwa ada nyinginezo ambazo hazijaidhinishwa na Wizara ya Elimu.

Kutokana na ada hizo za ziada kuna baadhi ya shule za upili za kitaifa ambapo mwanafunzi atahitajika kulipa zaidi ya Sh80,000 kwa mwaka, kutoka kiwango rasmi cha Sh53,000.

  • Tags

You can share this post!

Joto lazidi kuhusu Mama Ngina

Gusa Uhuru uone, Raila aonya Ruto

T L