• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Walioathiriwa na wanyamapori eneo la Masimba waitaka serikali iwalipe fidia

TUSIJE TUKASAHAU: Walioathiriwa na wanyamapori eneo la Masimba waitaka serikali iwalipe fidia

HAZINA ya Kitaifa inapaswa kutenga fedha kila mwaka za kushughulikia wanaothiriwa na mizozo kati ya binadamu na wanyamapori.

Hii ni kwa sababu Sheria ya Fidia kwa Wanaoshambuliwa na Wanyamapori ilianza kutekelezwa Novemba 2013 baada ya kutiwa saini na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.

Ni kwa misingi ya sheria hii ambapo mnamo Julai 14, 2022, aliyekuwa Waziri wa Usalama, Dkt Fred Matiang’i, aliwaahidi wakazi wa Kajiado walioshambuliwa na wanyamapori kwamba wangelipwa fidia.

Alisema kuwa Hazina ya Kitaifa ilikuwa imetoa Sh1.5 bilioni za kuwalipa wakazi wa eneo la Masimba, eneobunge la Kajiado Mashariki, Kaunti ya Kajiado.

Hii ni baada ya eneo hilo kushuhudia ongezeko la visa vya binadamu kushambuliwa na wanyamapori.

Hata hivyo, hadi sasa waathiriwa wa visa hivyo hawajapata fidia hiyo.

Sasa wanamkumbusha Mbunge wao, Bw Kakuta Maimai, kuwasilisha kilio chao kwa wizara husika ya serikali ili walipwe fidia walioahidiwa na utawala uliopita.

  • Tags

You can share this post!

Usalama waimarishwa Bondeni mitihani iking’oa nanga

MWALIMU WA WIKI: Mbunifu, mtafiti na mwajibikaji pia

T L