• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Wapi Baraza la Kiswahili la Kenya?

TUSIJE TUKASAHAU: Wapi Baraza la Kiswahili la Kenya?

MNAMO Agosti 14, 2018 Baraza la Mawaziri chini ya uenyekiti wa Rais Uhuru Kenyatta liliidhinisha kuundwe Baraza la Kiswahili la Kenya (BAKIKE).

Baraza hilo lingetwikwa wajibu wa kutunga sera za kuendeleza na kukuza lugha hii ya kitaifa na rasmi nchini kwa mujibu wa Katiba ya sasa. Baraza hilo pia lingehakikisha shughuli za asasi mbalimbali zinaendeleza mipango ya ukuzaji Kiswahili nchini.

Lakini, Alhamisi wiki jana baraza la mawaziri lilipofanya mkutano wa kwanza ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu, suala hilo muhimu halikujadiliwa.

Rais Kenyatta ameonekana kusahau mawaziri walipitisha uamuzi wa kuundwa kwa BAKIKE zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Huenda kuchelewa kuundwa kwa baraza hili ama ni wa kimakusudi au waliotwikwa jukumu hilo katika Wizara ya Michezo, Turathi na Utamaduni, wamezembea kazini au hawaoni umuhimu wake.

Hii ni licha ya Kiswahili kuendelea kuthaminiwa katika ngazi za kimataifa kwani juzi Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi na Utamaduni (UNESCO), lilitangaza kuwa Julai 7 itakuwa Siku ya Kiswahili Duniani, kila mwaka.

Aidha, juzi Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ilitangaza Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kuendeshea shughuli zake.

  • Tags

You can share this post!

Hofu pesa za wizi zinapaka tope uchaguzi

Wanjigi achagua wakili mwaniaji mwenza

T L