• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Wanjigi achagua wakili mwaniaji mwenza

Wanjigi achagua wakili mwaniaji mwenza

NA JURGEN NAMBEKA

MFANYABIASHARA na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Safina amemteua wakili Willis Otieno, kuwa mgombea mwenza wake katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua mgombea mwenza katika hoteli ya Ufungamano jijini Nairobi, alieleza kuwa amemchagua Bw Willis kwa sababu ni rafiki wa karibu.

Mwaniaji huyo wa urais alimtaja Bw Otieno kuwa aliyefaa zaidi, huku akimpa sifa kwa kuwa kielelezo bora kwa Wakenya wenye umri wa miaka 40 kurudi chini.

“Nimemchagua ndugu yangu hapa kwasababu yeye ndiye atakayenifaa. Hatua ya kumchagua ilikuwa rahisi sana. Ninamfahamu vyema kwa kuwa ni rafiki wa karibu,” alisema Bw Wanjigi.

Akitetea hali yake na Bw Otieno kutokuwa na tajriba ya kuendesha nchi, alisema kuwa hata Rais Mstaafu Mzee Jomo Kenyatta aliongoza bila kuwa na tajriba.

“Wanasema eti wana tajriba ya juu. Sisi hatuna hiyo tajriba lakini tuko tayari kuanza upya,” alieleza Bw Wanjigi.

Bw Otieno ambaye ni mzawa wa Masumbi Kaunti ya Siaya, alikubali uteuzi wa Bw Wanjigi akisema kuwa yupo tayari kukabiliana na Dkt Ruto, na Bw Odinga Agosti 9.

“Ninapokea uteuzi huu kwa ujasiri mwingi. Kijana wa kijijini amepewa nafasi ya kubadilisha maisha ya Wakenya,” alisema Bw Otieno.

Bw Wanjigi aliwapiga vijembe wapeperusha bendera wa miungano ya Kenya Kwanza Dkt William Ruto na mwenzake wa Azimio la Umoja, akisema kuwa wanaendeleza hatamu ya chama cha Jubilee ambayo imewaumiza Wakenya.

“Hawa ndugu zangu wanasema watapeana Sh6,000 na mabilioni kwa mama mboga. Ukweli ni kwamba nchi ina madeni. Hakuna pesa za kupeana,” alisema Bw Wanjigi.

  • Tags

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Wapi Baraza la Kiswahili la Kenya?

Mahakama yaagiza mwanamume, 52, arudishiwe mahari baada ya...

T L