• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
STEVE ITELA: Uhifadhi wa mazingira si hatia na wanaharakati wote wanafaa kulindwa

STEVE ITELA: Uhifadhi wa mazingira si hatia na wanaharakati wote wanafaa kulindwa

Na STEVE ITELA

MNAMO Julai 15, 2021 mwanamazingira Joannah Stutchbury aliuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake katika kile kinachoonekana kuwa mauaji.

Joannah Stutchbury alikuwa mtetezi mkuu wa mazingira na mhifadhi, ambaye alifahamika mno kwa juhudi zake za kuyalinda mazingira.

Alikuwa mkazi wa Kaunti ya Kiambu, akiishi karibu na hifadhi ya Msitu ya Kiambu. Hapo, alijulikana kwa kujitolea mhanga kuuhifadhi na kuulinda msitu dhidi ya unyakuzi wa ardhi na shughuli haramu.

Kifo cha Joannah kilikuwa sawa na cha Dkt Esmond Bradley Martin, mwanamazingira aliyekuwa akichunguza biashara ya pembe za ndovu na faru, katika harakati za kuwalinda wanyama walio katika hatari ya kuangamia.

Dkt Martin alipatikana akiwa ameuawa kwa kudungwa visu nyumbani kwake mtaa wa Karen, Nairobi. Hadi leo, hakuna habari zozote kuhusu waliohusika na kifo chake.

Kutokana na kuendelea kuharibiwa kwa mazingira na wanyamapori, wikendi wanamazingira walitembea kwa kilomita tatu katika msitu wa Kiambu. Walizungumza kuhusu changamoto wanazokumbana nazo na wakajadili jinsi ya kuzitatua. Baadaye walipanda miti na kuweka mabango yaliyo na ujumbe na namba za kupiga simu kuripoti visa vyovyote vya uharibifu ndani ya msitu huo.

Walizungumza na kutoa mapendekezo manne, ambayo nakubaliana nayo. Mambo hayo yafaa yashughulikiwe mara moja.

Kwanza, Bi Stutchbury apewe hadhi na atambuliwe kuwa mwanamazingira aliyejitolea. Bunge liunde sheria za kuwalinda wanaotetea mazingira; kuwe na sheria itakayowakabili na kuwaadhibu watakaoharibu au kuingilia juhudi za kuhifadhi mazingira.

Na mwisho, serikali ihakikishie umma kwamba maeneo yote yenye misitu au chemichemi za maji, yanalindwa dhidi ya wanyakuzi.

Uhifadhi wa mazingira si uhalifu.

Ni jambo linalosisitizwa na Katiba yetu. Kwan hivyo wanamazingira wanahitaji kulindwa kama Wakenya wengine kama inavyosema katiba. Wakenya wanaopigania kulinda maeneo machache ya msitu yaliyosalia, kuhakikisha kwamba tuna mazingira salama ya kuishi, wanaendelea kutishwa na kuhangaishwa.

  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Kipindi kigumu kwa walio na HIV na TB

JIJUE DADA: Kuzuia ngozi kuzeeka mapema

T L