• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 3:09 PM
WANDERI KAMAU: Mrithi wa Uhuru aendeleze uhuru wa kujieleza na demokrasia

WANDERI KAMAU: Mrithi wa Uhuru aendeleze uhuru wa kujieleza na demokrasia

NA WANDERI KAMAU

LICHA ya changamoto za kisiasa na kiuchumi zinazotuandama kama nchi, angaa kuna matumaini kuwa demokrasia yetu inaendelea kustawi.

Kenya imepiga hatua kubwa sana kidemokrasia ikilinganishwa na mataifa jirani kama Uganda, Somalia, Sudan Kusini, Ethiopia, Burundi na Rwanda.

Changamoto zetu kamwe haziwezi kulinganishwa na yale wanayopitia raia wa Uganda.

Hapa Kenya, wananchi huwa na uhuru wa kufanya maandamano, kuikosoa serikali watakavyo, kuchapisha jumbe tofauti katika mitandao ya kijamii bila kuogopa lolote kati ya mengine.

Ingekuwa ni katika baadhi ya nchi zilizotajwa hapo juu, pengine wakosoaji wote wa serikali wangekuwa wameshafungwa gerezani.

Msingi huu wa uhuru wa kujieleza uliwekwa na hayati Rais Mwai Kibaki, alipochukua uongozi mnamo 2003.

Hapo awali, ilikuwa vigumu kwa yeyote kueleza maoni yake kwa njia huru bila kuogopa kukamatwa.

Ni mtindo ulioifanya serikali ya marehemu Daniel Toroitich arap Moi kuogopwa na Wakenya wengi—hasa wanahabari, mawakili, watetezi wa haki za umma na wahadhiri.

Utawala huo ulichukulia ukosoaji wowote kama “kukosewa heshima”.Alipochukua uongozi mwaka wa 2013 kutoka kwa Rais Kibaki, Rais Uhuru Kenyatta ameendeleza mtindo huo.Kwa kiwango kikubwa, kila mmoja amekuwa huru kujieleza bila kuogopa kukabiliwa na vikosi vya serikali.

Hivyo, wito mkuu ni kwa kiongozi ambaye atachukua usukani baada ya Rais Kenyatta hapo Agosti kuendeleza uhuru huo ili kuistawisha demokrasia hata zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Wawaniaji huru kuteua mmoja wao kuwawakilisha katika...

Polisi wapewa idhini ya kupiga risasi na kuua wahalifu wa...

T L