• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
WANDERI KAMAU: Vyama vinavyowapunja wawaniaji vinafaa kukabiliwa vikali kisheria

WANDERI KAMAU: Vyama vinavyowapunja wawaniaji vinafaa kukabiliwa vikali kisheria

NA WANDERI KAMAU

KWA majuma kadhaa sasa, ulingo wa siasa nchini umegeuka kuwa jukwaa la machozi, vilio na majuto kwa wawaniaji wengi wanaoraiwa na vyama vya kisiasa kuacha kuwania nyadhifa walizolenga kuwania Agosti, na badala yake kuwaunga mkono watu wengine.

Cha kusikitisha ni kuwa, baadhi ya wawaniaji wanaambiwa kufanya hivyo wakati washalipa ada za uteuzi ili kupewa vyeti na vyama husika.

Kwa tathmini fupi, huwa inamgharimu mwaniaji maelfu ya pesa kupata cheti cha kuwania nyadhifa kama vile ugavana, useneta au ubunge.

Kwa mfano, wale wanaowania ugavana wanahitajika kulipa ada ya hadi Sh500,000 ili kupewa vyeti na vyama hivyo.

Ada za ubunge na useneta ni kati ya Sh200,00 na Sh300,000.

Kuutia msumari kwenye kidonda, mtindo huu hauendeshwi tu na vyama vikubwa vya kisiasa kama vile UDA, ODM ama Jubilee; bali pia na vyama vidogo vilivyobuniwa majuzi.Kumeibuka madai kwamba baadhi ya vyama hivyo vimebuni mtindo wa kuwarai wawaniaji waliopata tiketi zake “kujiondoa” na kuwaunga mkono wawaniaji wa vyama vingine mara tu baada yao kulipa ada ili kupewa vyeti hivyo.

Wengi wanalalama kuwa juhudi zao kuwafikia viongozi wa vyama hivyo hazifaulu hata kidogo.

Bila shaka, ni wazi kuwa mtindo huo umevigeuza vyama hivyo kuwa jukwaa la utapeli na unyang’anyi kwa mamia ya Wakenya wanaolenga kujitosa kwenye ulingo wa siasa.

Wito mkuu ni kwa Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa: tafadhali waokoe Wakenya dhidi ya ulaghai huo kwa kuhakikisha vyama vinavyosajiliwa vinazingatia taratibu zote za kisheria zilizowekwa.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Kashfa ambazo zilipaka tope utawala wa Rais Kibaki

Barobaro aeleza jinsi alivyofaidika na elimu bila malipo

T L