• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 10:44 AM
WANDERI KAMAU: Wakati wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ni sasa

WANDERI KAMAU: Wakati wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ni sasa

Na WANDERI KAMAU

SUALA la mabadiliko ya hali ya hewa limeibuka kuwa miongoni mwa midahalo mizito zaidi inayoendelea katika sehemu mbalimbali duniani.

Juhudi za kukabili athari za mabadiliko hayo ndizo zilikuwa ajenda kuu la kongamano lililokamilika majuzi katika jiji la Glasgow, Scotland. Suala lilo hilo ndilo lilikuwa kaulimbiu ya Kongamano la Saba la Ugatuzi lililokamilika jana katika Kaunti ya Makueni.

Swali kuu linaloibuka ni: Je, kuna mikakati maalum inayowekwa na wadau husika ama ni matamshi na hotuba tamu zinazotolewa bila hatua zozote kuchukuliwa?Sababu kuu ya urejeleo huo ni kutokana na athari ambazo zinaendelea kudhihirika kote kote duniani kuhusiana na hali hiyo.

Tangu mwaka uliopita, mamilioni ya watu nchini na katika eneo la Afrika Mashariki wameachwa bila chakula cha kutosha, baada ya mamilioni ya nzige kuvamia mashamba yao na kuharibu karibu mazao yote waliyokuwa wamepanda.Pili, watu wanaoishi karibu na maziwa kama Baringo, Naivasha, Elementaita kati ya mengine eneo la Bonde la Ufa, wanakabiliwa na hatari kubwa kutokana na kupanda kwa kiwango cha maji katika maziwa hayo.

Kwa sasa, watu zaidi ya 2.5 milioni katika kaunti karibu 20 nchini wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na kiangazi cha muda mrefu. Bila shaka, ni wazi matatizo hayo—kati ya mengine mengi—yanatokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.Huu ni wakati wa vitendo kwa wadau wote duniani. Hili ni janga linalohatarisha maisha ya kila mmoja.

[email protected]

You can share this post!

Ruto asusia Kongamano la Ugatuzi

DOUGLAS MUTUA: Vigogo wa kisiasa wasitumie kesi ICC...

T L