• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
WANTO WARUI: Wabunge watunge sheria kukinga mfumo wa elimu kuvurugwa kiholela

WANTO WARUI: Wabunge watunge sheria kukinga mfumo wa elimu kuvurugwa kiholela

Kila mtu kote nchini anaelewa umuhimu wa kuwa na elimu bora. Taifa likikosa wasomi wazuri litajipata pabaya. Litakosa watendakazi mahiri katika sehemu mbalimbali za kukuza uchumi na kuchuma mali.

Kwa mfano, kazi nyingi zinazoleta maendeleo nchini hutegemea viongozi waliosoma, walimu, madaktari, wahandisi,wachoraji ramani, majaji na kadhalika.

Elimu inapokosa kuwa imara, basi kutakuwa na shida nyingi siku za usoni.

Hii ndiyo sababu wabunge sasa wanahitaji kuanza matayarisho ya miswada itakayokinga elimu dhidi ya kuingiliwa kiholela na wanasiasa.

Kwa mfano, masomo hayahitaji kusimamishwa ghafla ili kuipa sekta nyingine fursa ya kufanya mambo yake kama tulivyoshuhudia katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Shughuli kama hizo za uchaguzi zinaweza kufanyiwa katika sehemu nyingine kama vile makanisani, kumbi za mikutano au katika viwanja vilivyo wazi.

Wanafunzi hawafai kukatiziwa masomo yao kwa shughuli kama hizi. Aidha, kumekuwa na shaka na malalamishi katika utendakazi wa sekta ya elimu, ikiongozwa na Waziri wa Elimu George Magoha.

Waziri amekuwa akitoa maamuzi muhimu yanayohusu watoto wengi barabarani huku mengine yakiwa yanakanganya walimu na wazazi.

Kwa sasa, ni vyema wabunge watambue vyema kuwa kati ya mabadiliko yanayohitajika pakubwa nchini ni kuikinga sekta ya elimu dhidi ya kuingiliwa ovyo ovyo na viongozi wetu wa kisiasa.

  • Tags

You can share this post!

Asukumwa jela miaka 4 kwa kuiba pombe kali

Nafuu kwa Arsenal nyota wao watatu wakitemwa katika kikosi...

T L