• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Asukumwa jela miaka 4 kwa kuiba pombe kali

Asukumwa jela miaka 4 kwa kuiba pombe kali

NA RICHARD MUNGUTI

MTAFUTA kazi aliyefumaniwa na polisi akiiba pombe kali amesukumwa gerezani miaka minne.

Jackson Mwanzia alikabidhiwa kifungo hicho na hakimu mkazi Monica Maroro alipokiri shtaka la kuvunja kilabu na kuiba pombe kali.

Mwanzia alikiri kuvunja duka la Rose na kuiba pombe na spika za redio zinazovurumisha muziki walevi wakibugia pombe.

Bi Maroro alielezwa Mwanzia alikutwa na polisi ndani ya duka hilo la kuuza vileo akiwa na aina mbalimbali za pombe.

Spika ya kuporomosha muziki aliyoiba ni ya thamani ya Sh2,500.

Hakimu alielezwa thamani ya pombe iliyoibwa ni Sh11,910.

Pia aliiba birika la kuchemsha maji lenye thamani ya Sh1,500.

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha Akila waliokuwa wanashika doria eneo la Nairobi West walipashwa habari za wizi uliokuwa unaendelea.

Walimkamata mshtakiwa lakini mwenzake alichomoka mbio.

Mwanzia alikamatwa akiwa na pombe aina ya Johnny Walker, Jack Daniels, Richot na Gilbeys miongoni mwa aina nyinginezo alizoiba.

Akijietetea Mwanzia alieleza korti anasaka kazi na kwamba ameoa na amejaliwa kupata watoto watatu.

Mfungwa huyo alipewa siku 14 kukata rufaa.

  • Tags

You can share this post!

KIGODA CHA PWANI: Ni nani atakuwa macho na masikio ya Rais...

WANTO WARUI: Wabunge watunge sheria kukinga mfumo wa elimu...

T L