• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Mwanamke ni shujaa

Mwanamke ni shujaa

Na Assumptah Wausi

Mwanamke ni shujaa , biashara kakamka

Si wa jikoni malkia, hakika amechupuka

Tafuta ametambua, ki fedha anafaidika

Mwanamke kawa taa, na mlezi kadhalika 

 

Mwanamke chanjamaa, tia bidii hakika

Ziko nyingi vibarua, jaribu utainuka

Fanya kazi injinia, pesa benki weka

Mwanamke kawa taa, na mlezi kadhalika .

 

Mwanamke karibia, kasumba acha haraka

Uza andazi kofia , jitahidi na damka

Yaache ya chekechea, changamana kamilika

Mwanamke kawa taa, na mlezi kadhalika.

 

Mwanamke chokonoa, mwenzako nafasi nyaka

AWE kawa msaada, heko kote utawika

Mwanga wa familia , kurunzi pote limbika

Mwanamke kawa taa, na mlezi kadahalika.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Maji ya Ziwa Victoria yasababisha kansa, watahadharisha...

WANDERI KAMAU: Changamoto tele Mlima ukijaribu kuja pamoja

T L