• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 5:45 AM
Akumu na klabu yake ya Kaizer Chiefs wapigwa kwenye fainali ya CAF, wazoa Sh136 milioni

Akumu na klabu yake ya Kaizer Chiefs wapigwa kwenye fainali ya CAF, wazoa Sh136 milioni

Na GEOFFREY ANENE

KAIZER Chiefs anayochezea Mkenya Anthony “Teddy” Akumu imeridhika na tuzo ya Sh136,141,871 baada ya kulemewa na Al Ahly kutoka Misri 3-0 katika fainali ya Klabu Bingwa Afrika mnamo Julai 17.

Al Ahly, ambao wamefuzu kushiriki Kombe la Klabua Bingwa Duniani, walitia kibindoni Sh272,283,743.

Miamba hao wa kutoka Soweto, ambao walitumia kiungo huyo mkabaji wa Harambee Stars katika dakika 32 za mwisho alipojaza nafasi ya beki Njabulo Blom, walikamilisha kipindi cha kwanza bila kufungwa bao.

Hata hivyo, Chiefs walienda mapumzikoni wakiwa watu 10 baada ya Happy Mashiane kuonyeshwa kadi nyekundu.

Vijana wa kocha Stuart Baxter walihangaishwa na miamba hao katika kipindi cha pili ugani Mohamed V jijini Casablanca, Morocco.

Al Ahly, ambayo inanolewa na kocha Pitso Mosimane kutoka Afrika Kusini, ilinyakua taji lake la 10 la Klabu Bingwa baada ya kupata mabao yake kupitia kwa Mohamed Sherif dakika ya 53, Magdy Afsha (64) na Amr El Solia (74).

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Kura si mwisho wa maisha, tulinde utu

Vieira aanza kazi kambini mwa Palace kwa ushindi dhidi ya...