• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 6:55 AM
Amerika kuwa mwenyeji wa kipute kilichopanuliwa cha Klabu Bingwa Duniani 2025

Amerika kuwa mwenyeji wa kipute kilichopanuliwa cha Klabu Bingwa Duniani 2025

Na MASHIRIKA

AMERIKA watakuwa wenyeji wa kipute kilichopanuliwa cha Klabu Bingwa Duniani ambacho kitajumuisha timu 32 za wanaume mnamo 2025, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limethibitisha.

Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema mashindano hayo yatakuwa kilele cha michuano ya soka miongoni mwa wanaume.

Jumla ya klabu 12 za bara Ulaya zitashirikishwa, wakiwemo washindi watatu waliopita wa taji la Klabu Bingwa Ulaya – Chelsea, Real Madrid na Manchester City.

Tarehe za kufanyika kwa kipute hicho hazijathibitishwa japo mashindano yenyewe yanatarajiwa kusakatwa mwezi Juni 2025.

Amerika watashirikiana na Canada na Mexico kuwa wenyeji wa fainali zijazo za Kombe la Dunia mnamo 2026.

Makala ya 20 ya Klabu Bingwa Duniani yatafanyika kati ya Disemba 12-22, 2023 nchini Saudi Arabia.

Real Madrid walishinda makala yaliyopita ya kipute hicho kilichofanyika nchini Morocco mnamo Februari 2023. Taifa hilo la bara Afrika liliandaa mashindano hayo tena mnamo 2013 na 2014. Mataifa mengine ambayo yamewahi kuwa wenyeji wa Klabu Bingwa Duniani ni Brazil, Japan, UAE na Qatar.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mtindo wa wahalifu kurudia makosa waendelee kufurahia...

Wafuasi wa Jicho Pevu wakabiliana na wenzao wa Hassan Omar

T L