• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 6:50 AM
Arsenal kufika mwisho wa lami wakiteleza dhidi ya Nottingham Forest

Arsenal kufika mwisho wa lami wakiteleza dhidi ya Nottingham Forest

NA MASHIRIKA

LONDON, Uingereza:

BINGWA wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu 2022-2023 huenda akajulikana Jumamosi iwapo safari ya Arsenal katika klabu ya Nottingham Forest itaishia kwa kichapo ama sare.

Wanabunduki wa Arsenal wanakamata nafasi ya pili kwa pointi 81 baada ya kujibwaga uwanjani mara 36. Wako pointi nne nyuma ya viongozi na mabingwa watetezi Manchester City ambao wamesakata mechi moja chache.

Vijana wa kocha Mikel Arteta wangali na nafasi ya kutwaa ubingwa, ingawa ni finyu sana.

Wanahitaji kulipua Nottingham mnamo Jumamosi na Wolves mnamo Mei 28 na kuomba miujiza ifanyike kambini mwa City ya kupoteza dhidi ya Chelsea (Mei 21), Brighton (Mei 24) na Brentford (Mei 28).

Kuna nafasi kubwa City itashinda taji lake la tano katika kipindi cha miaka sita itakapokutana na wanyonge Chelsea mnamo Jumapili jioni.

Vijana wa kocha Pep Guardiola hawashikiki. Watafukuzia ushindi wa 12 mfululizo ligini kesho.

Arsenal huenda wakatunuku City ubingwa wa ligi ikiwa watateleza dhidi ya Nottingham inayotarajiwa kujituma kwa sababu ipigana kufa-kupona kuepuka kushushwa ngazi.

Kocha wa Nottingham, Steve Cooper anatarajiwa kuwa na huduma za Danilo na Emmanuel Dennis kutoka mkekani. Washambulizi Taiwo Awoniyi na Brennan Johnson ni baadhi ya silaha Arsenal watalazimika kuzima wasipatwe na madhara.

Arteta hatarajiwi kuwa na huduma za mvamizi Gabriel Martinelli aliyeumia dhidi ya Brighton pamoja na mabeki Oleksandr Zinchenko na William Saliba.

Leandro Trossard na Martin Odegaard ni baadhi ya vifaa Arsenal itatumia kutafuta matokeo mazuri.

Jumla ya mechi sita zitasakatwa Jumamosi ambapo Liverpool itaing’oa Manchester United kutoka nne-bora ikilima Aston Vila nao vijana wa kocha Erik ten Hag wajikwae dhidi ya Bournemouth.

Aidha, nambari tatu Newcastle ilipiga hatua kubwa katika juhudi za kufuzu kushiriki Klabu Bingwa Ulaya baada ya kupepeta Brighton 4-1 kupitia mabao ya Deniz Undav (alijifunga), Dan Burn, Callum Wilson na Bruno Guimaraes, Alhamisi. Undav alifungia Brighton bao la kufuta machozi.

Ratiba:

Mei 20

Tottenham v Brentford (2.30pm), Liverpool v Aston Villa (5.00pm), Wolves v Everton (5.00pm), Bournemouth v Manchester United (5.00pm), Fulham v Crystal Palace (5.00pm), Nottingham Forest v Arsenal (7.30pm);

Mei 21

West Ham v Leeds (3.30pm), Brighton v Southampton (4.00pm), Manchester City v Chelsea (6.00pm);

Mei 22

Leicester (10.00pm);

Mei 24 – Brighton v Manchester City (10.00pm);

Mei 25 – Manchester United v Chelsea (10.00pm).

  • Tags

You can share this post!

Shakahola: Wanahabari wanyimwa fursa kuangazia mazungumzo...

Akothee afichua kuanza kumeza dawa za kusaidia kushika...

T L