• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Auba mali ya Chelsea dakika za lala salama

Auba mali ya Chelsea dakika za lala salama

NA MASHIRIKA

LONDON, UINGEREZA

KLABU za Ligi Kuu Uingereza (EPL) zimekuwa na shughuli nyingi zikitumia zaidi ya Sh236.2 bilioni kununua wachezaji toka soko lifunguliwe Juni 10 hadi Septemba 1 lilipofungwa.

Klabu za EPL zilitumia Sh200.1 bilioni sokoni msimu uliopita.

Baadhi ya majina makubwa yameingia EPL msimu 2022-2023 ni pamoja na nyota wa zamani wa Arsenal Pierre-Emerick Aubamenyang kujiunga na Chelsea kutoka Barcelona, kinda matata Erling Haaland kuwa mali ya mabingwa watetezi Manchester City akitokea Borussia Dormund, Casemiro kutua Manchester United kutoka Real Madrid na Gabriel Jesus kuyoyomea Arsenal kutoka Manchester City. Liverpool pia ilipata huduma za Darwin Nunez kutoka Porto.

Sajili za siku ya mwisho

Hizi hapa ni sajili zilizofanywa siku ya mwisho: Anthony – Ajax hadi Manchester United (Sh11.9 bilioni), Manuel Akanji – Borussia Dortmund hadi Manchester City (Sh2.0 bilioni), Wout Faes – Reims hadi Leicester (Sh2.0 bilioni), Willy Boly – Wolves hadi Nottingham Forest (Sh646.2 milioni), Jack Stephens – Southampton hadi Bournemouth (mkopo), Idrissa Gueye – PSG hadi Everton (Sh1.1 bilioni), Willian – Corinthians hadi Fulham (bila ada ya uhamisho), Layvin Kurzawa – PSG hadi Fulham (mkopo), Martin Dubravka – Newcastle hadi Manchester United (mkopo), Leander Dendoncker – Wolves hadi Aston Villa (Sh1.8 bilioni), Ainsley Maitland-Niles – Arsenal hadi Southampton (mkopo), Sam Edozie – Manchester City hadi Southampton (Sh1.3 bilioni), Arthur Melo – Juventus hadi Liverpool (mkopo), James Garner – Manchester United hadi Everton (Sh2.0 bilioni), Juan Larios – Manchester City hadi Southampton (Sh833.6 million), Carlos Vinicius – Benfica hadi Fulham (haijafichuliwa), Jan Bednarek – Southampton hadi Aston Villa (mkopo), Duje Caleta-Car – Marseille hadi Southampton (Sh1.2 bilioni), Boubacar Traore – Metz hadi Wolves (mkopo), Dan James – Leeds hadi Fulham (mkopo), Loic Bade – Rennes hadi Nottingham Forest (mkopo), Wilfried Gnonto – FC Zurich hadi Leeds (bila ada ya uhamisho), Billy Gilmour – Chelsea hadi Brighton (Sh1.3 bilioni), Pierre-Emerick Aubameyang – Barcelona (Sh1.4 bilioni), Denis Zakaria – Juventus hadi Chelsea (mkopo).

  • Tags

You can share this post!

Conte: Ni wakati wa Kane kuongeza kandarasi yake

Barcelona wafaulu kumng’oa beki Marcos Alonso kambini...

T L