• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:50 AM
Azma ya Shujaa ni kujiinua Dubai 7s

Azma ya Shujaa ni kujiinua Dubai 7s

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande ya Kenya Shujaa inatarajiwa kuwa na kibarua kigumu inapolenga kuimarisha matokeo yake kwenye Raga za Dunia 2021-2022 zitakazoingia duru ya pili jijini Dubai mnamo Desemba 3-4.

Vijana wa Innocent Simiyu watakabana koo na Australia (8.44am), Amerika (2.20pm) na Canada (4.46pm) katika mechi za Kundi B hii leo. Shujaa ilikamata nafasi ya nane katika duru ya kwanza jijini Dubai mnamo Novemba 26-27 ikijizolea alama 10 kwenye msimu huu wa duru tisa.

Simiyu alieleza Taifa Leo hapo jana kuwa mazoezi yao juma hili yalilenga kurekebisha idara zilizosikitisha katika duru ya kwanza wikendi iliyopita. “Tumeimarisha mashambulizi yetu, jinsi ya kuanzisha mipira na umilikaji wa mpira. Lengo letu kubwa ni ni kuimarisha mchezo wetu katika idara zote matumaini yetu yakiwa ni kupata matokeo mazuri,” alisema Namcos.

. Timu zingine zinazoshiriki mashindano hayo ni Afrika Kusini, Great Britain, Ireland na Japan (Kundi A) na Argentina, Fiji, Ufaransa na Uhispania (Kundi C). Mabingwa wa Safari Sevens Shujaa walimaliza Raga za Dunia 2021 katika nafasi ya tatu nyuma ya Afrika Kusini na Great Britain.

You can share this post!

Tusker wazuru Tunis, huku Gor wakisubiri Congo

Nusu-fainali ya kukata na shoka

T L