• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Barcelona sasa pua na mdomo kutawazwa mabingwa wa La Liga kwa mara ya kwanza tangu 2019

Barcelona sasa pua na mdomo kutawazwa mabingwa wa La Liga kwa mara ya kwanza tangu 2019

Na MASHIRIKA

BARCELONA watatawazwa wafalme wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) msimu huu wa 2022-23 iwapo watatandika majirani zao Espanyol katika mchuano ujao mnamo Jumapili ya Mei 14, 2023.

Hii ni baada ya miamba hao kutandika Osasuna 1-0 mnamo Jumanne usiku kupitia bao la Jordi Alba ugani Camp Nou na kuendeleza udhibiti wao kileleni mwa jedwali la La Liga kwa alama 82 baada ya mechi 33.

Pengo la pointi 14 linatamalaki kati ya Barcelona na nambari mbili Real Madrid waliokubali kichapo cha 2-0 kutoka Real Sociedad ugenini.

Osasuna wanashikilia nafasi ya tisa jedwali kwa alama 44 sawa na nambari nane Girona. Walikamilisha mechi dhidi ya Barcelona wakiwa na wachezaji 10 pekee uwanjani baada ya Jorge Herrando kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumchezea Pedri Gonzalez. Kadi hiyo nyekundu ilikuwa ya saba kwa Osasuna kupokezwa katika La Liga msimu huu wa 2022-23.

Zikiwa zimesalia mechi tano pekee kwa kampeni za msimu huu wa La Liga kutamatika rasmi, Barcelona wanaonolewa na kocha Xavi Hernandez wanahitaji kushinda pambano moja pekee ili kutawazwa wafalme wa kipute hicho kwa mara ya kwanza tangu 2019.

Osasuna walifanyia kikosi chao dhidi ya Barcelona mabadiliko tisa kadri wanavyojiandaa sasa kuvaana na Real kwenye fainali ya Copa del Rey mnamo Mei 6, 2023 jijini Seville, Uhispania.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mafuriko: Wakazi wa Mukuru walazimika kutumia daraja kabla...

Washambulizi Harambee Starlets wang’aa TZ na Rwanda

T L