• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 7:52 PM
Barcelona wapaa hadi nafasi ya saba baada ya kupepeta Elche ligini

Barcelona wapaa hadi nafasi ya saba baada ya kupepeta Elche ligini

Na MASHIRIKA

MWANASOKA Nico Gonzalez alifungia Barcelona bao mwishoni mwa kipindi cha pili na kusaidia waajiri wake hao kupepeta Elche 3-2 katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) mnamo Jumamosi.

Ferran Jutgla aliwafungulia wenyeji Barcelona ukurasa wa mabao katika dakika ya 16 kabla ya chipukizi Paez Gaviria, 17, kufanya mambo kuwa 2-0 baada ya kupachika wavuni goli lake la kwanza katika soka ya La Liga.

Hata hivyo, Tete Morente na Pere Milla walitokea benchi katika kipindi cha pili na kufungia Elche mabao mawili ya haraka katika dakika za 62 na 63 ambayo yalisawazisha mambo.

Matokeo hayo yalisaza Barcelona ya kocha Xavi Hernandez katika nafasi ya saba jedwalini kwa alama 27, tatu nyuma ya Rayo Vallecano wanaokamata nafasi ya nne-bora na mbili pekee nyuma ya mabingwa watetezi Atletico Madrid waliopigwa 2-1 na Sevilla.

Ni pengo la pointi 15 ndilo linatamalaki kati ya Barcelona na viongozi Real Madrid wanaopigiwa upatu wa kutwaa taji la La Liga muhula huu chini ya kocha Carlo Ancelotti.

Barcelona walishuka dimbani wakilenga alama tatu muhimu baada ya kutoshinda mechi tatu za awali, ikiwemo nyingine iliyokamilika kwa sare ya 2-2 dhidi ya Osasuna mnamo Disemba 19, 2021 baada ya kupepetwa na Bayern Munich kwenye Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kisha dhidi ya Real Betis katika La Liga.

Kwa upande wao, Elche walisalia katika nafasi ya 16 kwa alama 15 sawa na Alaves. Ni pengo la alama tano ndilo linatenganisha viongozi Real Madrid na nambari mbili Sevilla waliokomoa Atletico Madrid 2-1.

MATOKEO YA LA LIGA (Jumamosi):

Barcelona 3-2 Elche

Sevilla 2-1 Atletico

Vallecano 2-0 Alaves

Sociedad 1-3 Villarreal

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Matumaini tele daraja la Ngoliba likikaribia kukamilika

FA yapiga Leeds United faini ya Sh3 milioni kwa utovu wa...

T L