• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 2:33 PM
Batshuayi arefusha mkataba wake kambini na Chelsea na kutua Besiktas

Batshuayi arefusha mkataba wake kambini na Chelsea na kutua Besiktas

Na MASHIRIKA

FOWADI Michy Batshuayi amejiunga na Besiktas ya Ligi Kuu ya Uturuki kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu wa 2021-22 baada ya kurefusha mkataba wake na Chelsea hadi 2023.

Mkopo huo ni wa tano kwa Batshuayi tangu ajiunge na Chelsea mnamo 2016.

Nyota huyo raia wa Ubelgiji amewahi pia kuchezea Borussia Dortmund na Valencia kwa mkopo wa msimu mmoja kabla ya kusakatia Crystal Palace kwa misimu miwili ambapo alifunga mabao mawili kutokana na mechi 18 za muhula uliopita wa 2020-21.

Batshuayi hajawahi kuchezea Chelsea katika mchuano wowote tangu Februari 2020 na amefungia kikosi hicho jumla ya mabao 25 kutokana na mechi 77 tangu asajiliwe kutoka Olympique Marseille ya Ufaransa kwa Sh5 bilioni.

Besiktas walitawazwa wafalme wa Ligi Kuu ya Uturuki (Super Lig) mnamo 2020-21 na watanogesha kampeni za Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo 2021-22.

Japo Batshuayi alifungia Chelsea mabao sita pekee mnamo 2019-20 chini ya kocha Frank Lampard, alikosa nafasi za kuwajibikia kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa Tammy Abraham na Olivier Giroud ambao kwa sasa wamejiunga na AS Roma na AC Milan za Italia mtawalia.

Batshuayi alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshindia Chelsea ufalme wa EPL mnamo 2016-17 chini ya mkufunzi Antonio Conte.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Manuel Locatelli wa Italia ajiunga na Juventus

Celtic wakung’uta AZ Alkmaar kwenye mchujo wa Europa...