• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Benfica wakomoa Juventus na kuendeleza masaibu ya kocha Massimiliano Allegri jijini Turin

Benfica wakomoa Juventus na kuendeleza masaibu ya kocha Massimiliano Allegri jijini Turin

Na MASHIRIKA

JUVENTUS walipokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa Benfica katika mechi ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) iliyomzidishia kocha Massimiliano Allegri presha ya kupigwa kalamu jijini Turin.

Juventus kwa sasa wamepoteza mechi mbili mfululizo za UEFA katika Kundi H na wanakabiliwa na mtihani mgumu wa kutinga hatua ya 16-bora.

Wakitawaliwa na kiu ya kushinda, Juventus waliwekwa kifua mbele na Arkadiusz Milik katika dakika ya 14 kabla ya Joao Mario kurejesha Benfica mchezoni kupitia mkwaju wa penalti mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

David Neres alifungia Benfica bao la ushindi ugani Allianz katika dakika ya 55 na kuendeleza masaibu ya Juventus waliopigwa na PSG 2-1 katika mechi ya kwanza mnamo Septemba 6, 2022. Ni mara ya kwanza katika historia kwa Juventus kupoteza mechi mbili mfululizo za UEFA katika hatua ya makundi.

Kikosi hicho kimeshinda mechi mbili pekee kati ya sita za kwanza katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) msimu huu wa 2021-22 na kinakamata sasa nafasi ya nane jedwalini kwa alama nne nyuma ya viongozi Napoli.

Kwa upande wao, Benfica wameshinda mechi zote 12 za ufunguzi wa msimu huu na ushindi dhidi ya Juventus ulikuwa wao wa kwanza kusajili nchini Italia tangu 1997.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Gachagua awasamehe wote na kukumbatia...

Jinsi unavyoweza kupunguza uzito na kuboresha afya

T L