• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:55 AM
Bingwa wa marathon Chepng’etich kivutio Nairobi Cross Country

Bingwa wa marathon Chepng’etich kivutio Nairobi Cross Country

Na AYUMBA AYODI

MALKIA wa marathon wa Riadha za Dunia Ruth Chepng’etich atakuwa kivutio kwenye mbio za nyika za kaunti ya Nairobi katika uwanja wa Magereza wa Nairobi West mnamo Jumamosi.

Chepng’etich yuko katika orodha iliyo na bingwa mpya wa mbio za nyika za Elgoibar, Edinah Jebitok.

Zitakuwa mbio za kwanza za Chepng’etich mwaka 2022 tangu ashinde Chicago Marathon mnamo Oktoba 10 mwaka jana kwa saa 2:22:31.

Chepng’etich alikamata nafasi ya tatu katika mbio za nyika za kitaifa 2021 baada ya kumaliza nyuma ya mshindi Sheila Chelangat kutoka timu ya Police na Daisy Cherotich kutoka Central.

Jebitok alitwaa taji la Elgoibar nchini Uhispania mnamo Januari 9 akibwaga bingwa wa mbio za nyika za dunia za wakimbiaji wasiozidi umri wa miaka 20 mwaka 2019 Beatrice Chebet.

Mwaka 2021, Sandra alitawala mbio za nyika za Nairobi kwa dakika 33:48.7 akifuatiwa na dadake Emily Chebet (35:07.8).

Naibei Kiplimo kutoka Embakasi, ambaye alibeba taji la wanaume mbio za kilomita 10 mwaka jana, amerejea kulitetea.

Kiplimo, ambaye 2020 alikuwa nambari mbili, alishinda taji la 2021 kwa dakika 30:04.77.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Kenya (AK) tawi la Nairobi, Barnaba Korir alieleza Taifa Leo mnamo Ijumaa kuwa watatumia mashindano hayo kuchagua timu itakayoshiriki mbio za nyika za kitaifa Januari 22 uwanjani Lobo mjini Eldoret.

Mbio za kitaifa zitatumiwa kupima utayari wa Lobo kuandaa duru ya dunia ya Agnes Tirop mnamo Februari 12. TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

You can share this post!

Mainstream Academy balaa taji la Dago Super Cup

Malalamiko ya Nigeria yasababisha mashindano ya handiboli...

T L