• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:55 AM
Mainstream Academy balaa taji la Dago Super Cup

Mainstream Academy balaa taji la Dago Super Cup

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya Mainstream Academy imetawazwa mabingwa wa shindano la Dagoretti Super 2021-22 ambalo hufadhiliwa John Kiarie maarufu KJ ambaye ndiye mbunge wa Dagoretti Kusini.

Mainstream ya kocha, Kadiri Galgal imeibuka mabingwa wa kipute hicho baada ya kunyuka Dagoretti Youth mabao 3-0 kupitia mikwanju ya penalti baada ya kutoka nguvu sawa bao 1-1. Mchezo huo ulianza kwa kasi huku vijana wa Dagoretti Youth iliokuwa ikipigia chapuo kubeba taji hilo ilonesha mechi safi ndani ya dakika 20 za kwanza.

Hata hivyo Mainstream ilipofunga bao hali ilichukua mwelekeo mwingine. Wapinzani zote ziliendelea kupigana kwa udi na uvumba kabla ya Dagoretti Youth kusawazisha kunako dakika ya 80. Kwenye nusu fainali wapiga gozi wa Mainstream Academy walikanyanga Home in Home kwa mabao 3-0 nao vijana wa Dagoretti Youth ya kocha Simon Kamau ilibeba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Santos FC.

”Ninashukuru wachezaji wangu kwa kuonyesha ushirikiano mwema kwenye mechi hizo na hatimaye kuibuka mabingwa wa ngarambe ya mwaka huu ambayo ni makala ya tatu,” kocha wa Mainstream Academy, Kadiri Galgal alisema na kuongeza kuwa atazidi kulea na kukuza wachezaji wa soka katika kituo hicho.

”Kama kocha ningependa kushauri chipukizi wa michezo mbali mbali nchini watumie nafasi wanazopata vizuri hasa kupalilia vipaji vyao michezoni. kwa kipidni ambacho kimekuwa katika sekta ya mchezo wa spoti nimegundua kuwa fani hiyo imeajiri wengi kwa njia tofauti.” Kadhalika alidokeza kuwa michezo yote inahitaji wahusika kuonyesha nidhamu ya hali ya wakiwa ndani na nje ya uwanja.

Licha ya wafuasi wa Dagoretti Youth kuzua fujo kwenye mchezo huo kocha wake alikubali yaishe na kusema kuwa kwenye mchezo huo ilikuwa lazima mshindi apatikane.

Kwenye mechi za robo fainali, Mainstream Academy ilinyamazisha NYSA kwa mabao 5-4 kupitia mipigo ya penalti baada ya kutoka sare tasa katika muda wa kawaida. Wachana nyavu wa Santos FC walionyesha usongora wao kwakushinda Royal FC mabao 2-1, Dagoretti Youth ilizamisha Samwest Black Boots kwa mabao 3-2. Mwisho Makarios 111 (Riruta United) ilikubali yaishe ilipochapwa mabao 2-0 na Home in Home FC.

Kwenye nusu fainali ya wanaume, Mainstream Academy ilikanyanga Home in Home kwa mabao 3-0 nayo Dagoretti Youth ilibeba ushindi bao 1-0 mbele ya Santos. Mashindano ya mwaka ambayo ni makala ya tatu yalijumuisha timu 75 za wanaume na 12 za wanawake katika eneo bunge la Dagoretti Kusini.

Ngarambe hiyo ilishiriki timu kutoka Wadi zote tano katika eneo bunge hilo: Riruta, Mutuini, Waithaka, Ngando na Uthiru/Ruthimitu. Mashindano ya mwaka yalivutia jumla ya timu 75 ambapo mshindi alituzwa Sh100,000 huku nafasi ya pili ikipongezwa kwa Sh50,000. Mashindano mengi kuwania makombe tofauti huandaliwa kila mwanzo wa mwaka ambapo wachezaji wengi huyatumia kujiweka fiti kwa ajili ya mechi za ligi.

Wachezaji wa Mainstream Academy baada ya kupokezwa mabingwa wa kombe la Dagoretti Super Cup mwaka huu. …Picha/JOHN KIMWERE

You can share this post!

KIKOLEZO: Grammys zimebaki stori tu!

Bingwa wa marathon Chepng’etich kivutio Nairobi Cross...

T L