• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Carlos Tevez astaafu kwenye ulingo wa soka

Carlos Tevez astaafu kwenye ulingo wa soka

Na MASHIRIKA

FOWADI wa zamani wa Manchester United, Manchester City, West Ham United na timu ya taifa ya Argentina, Carlos Tevez, ameangika rasmi daluga zake katika ulingo wa soka.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 hajawahi kutandaza mchuano wowote tangu Juni 2021 alipokuwa akivalia jezi za kikosi chake cha tangu utotoni, Boca Juniors, kwa awamu ya tatu.

Alisema “amejituma vilivyo kitaaluma” katika kipindi cha miaka 20 iliyopita na matarajio yake yalikuwa kuendelea kutamba ulingoni.

Hata hivyo, kilichomchochea kustaafu licha ya kupokea ofa za kujiunga na vikosi mbalimbali vya haiba, ni kifo cha baba yake mzazi mwaka 2021.

Segundo Tevez aliaga dunia kutokana na Covid-19 mnamo Februari 2021 akiwa na umri wa miaka 58.

“Nimeacha kusakata kabumbu kwa sababu nilimpoteza babangu – shabiki wangu nambari moja. Ni rasmi kwamba sasa nimestaafu licha ya kuwasilishiwa ofa tele barani Ulaya na hata Amerika,” akasema Tevez.

Nyota huyo aliwahi pia kuchezea klabu za Juventus (Italia), Corinthians nchini Brazil na Shanghai Shenhua ya Ligi Kuu ya China.

Aliongoza Argentina kutwaa nishani ya dhahabu kwenye Olimpiki za 2004 nchini Athens, Ugiriki. Kufikia mwisho wa 2015, alikuwa amewajibishwa na mabingwa hao mara mbili wa dunia (1986, 1978) katika jumla ya mechi 75.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Lacazette kuondoka Arsenal mnamo Juni 30, 2022

ZARAA: Jinsi ushirikiano kati ya serikali na sekta ya...

T L