• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 11:50 AM
Lacazette kuondoka Arsenal mnamo Juni 30, 2022

Lacazette kuondoka Arsenal mnamo Juni 30, 2022

Na MASHIRIKA

FOWADI mzoefu raia wa Ufaransa, Alexandre Lacazette, 31, ataagana rasmi na Arsenal mnamo Juni 30, 2022 mkataba wake wa sasa ugani Emirates utakapotamatika.

Lacazette, 31, alijiunga na Arsenal mnamo Julai 2017 baada ya kuagana na Olympique Lyon wanaohusishwa na uwezekano mkubwa wa kujitwalia upya maarifa yake.

Lacazette alifungia Arsenal mabao 71 kutokana na mechi 206 na akanyanyulia kikosi hicho ufalme wa Kombe la FA mnamo 2020.

“Lacazette amekuwa mchezaji mahiri sana kambini mwetu. Amekuwa kiongozi wa kutegemewa ndani na nje ya uwanja na amechangia pakubwa kuwachochea chipukizi kadhaa kikosini,” akasema kocha Mikel Arteta.

Lacazette alifungia Arsenal mabao sita na kuchangia mengine manane katika jumla ya mechi 36 alizochezea Arsenal mnamo 2021-22.

Alipokezwa utepe wa unahodha kambini mwa Arsenal mnamo Disemba 2021 baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kutemwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Licha ya mchango mkubwa wa Lacazette, Arsenal walikamilisha kampeni zao za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu katika nafasi ya tano nyuma ya Tottenham Hotspur na hivyo kukosa fursa ya kunogesha kipute cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao wa 2022-23.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wazee waunga azma ya Kibwana kuwania useneta

Carlos Tevez astaafu kwenye ulingo wa soka

T L