• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:55 AM
Cesc Fabregas ajiunga na Como FC inayoshiriki Ligi ya Serie B nchini Italia

Cesc Fabregas ajiunga na Como FC inayoshiriki Ligi ya Serie B nchini Italia

Na MASHIRIKA

KIUNGO wa zamani wa timu ya taifa ya Uhispania, Cesc Fabregas, 35, amejiunga na klabu ya Como nchini Italia kwa mkataba wa miaka miwili.

Nyota huyo anajiunga na kikosi hicho cha Ligi ya Serie B nchini Italia baada ya mkataba wake kambini mwa AS Monaco nchini Italia kutamatika mnamo Juni 2022.

Fabregas aliingia katika sajili rasmi ya Monaco mnamo Januari 2019 baada ya kuagana na Chelsea. Alijiunga na kikosi hicho wakati ambapo kilikuwa kikonolewa na Thierry Henry aliyewahi kucheza naye pamoja katika klabu ya Arsenal.

“Nimekuwa na bahati kubwa zaidi kwa sababu taaluma hii ya usogora imenipa fursa ya kuvalia jezi za klabu za haiba kubwa, ikiwemo Como,” akasema Fabregas.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Como kwa sasa ni Dennis Wise aliyekuwa kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza.

Fabregas alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshindia Uhiapania Kombe la Dunia mnamo 2010 nchini Afrika Kusini. Alichezea Monaco mara 68 katika kipindi cha miaka mitatu na nusu iliyopita.

Aliwajibisha na Arsenal mara 212 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kati ya 2004 na 2011 kabla ya kuhamia Barcelona waliompokeza malezi ya soka katika akademia ya La Masia akiwa na umri wa miaka 10 pekee mnamo 1997.

Baada ya kusakata soka ya La Liga akivalia jezi za Barcelona kwa miaka mitatu, alirejea EPL kuwajibikia Chelsea waliomchezesha mara 200.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wafanyabiashara washiriki kongamano la maonyesho ya bidhaa...

Diogo Jota sasa kuchezea Liverpool hadi mwaka wa 2027

T L