• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Diogo Jota sasa kuchezea Liverpool hadi mwaka wa 2027

Diogo Jota sasa kuchezea Liverpool hadi mwaka wa 2027

Na MASHIRIKA

FOWADI matata wa Liverpool, Diogo Jota, 25, ametia saini mkataba mpya utakaomdumisha uwanjani Anfield hadi mwaka wa 2027.

Nyota huyo raia wa Ureno amefungia Liverpool mabao 34 kutokana na mechi 85 tangu abanduke kambini mwa Wolves kwa Sh5.9 bilioni mnamo 2020.

Alipachika wavuni mabao 21 mnamo 2021-22 na akaongoza Liverpool kunyanyua Kombe la FA na ubingwa wa Carabao Cup. Liverpool pia waliambulia nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Hadi aliporefusha muda wa kuhudumu kwake ugani Anfield, mkataba wa awali kati ya Jota na Liverpool ulikuwa utamatike mwaka wa 2025.

Mnamo Julai 2022, mshambuliaji mwingine wa Liverpool. Mohamed Salah, alitia saini mkataba wa miaka mitatu ugani Anfield baada ya mfumaji Sadio Mane kuyoyomea Ujerumani kuvalia jezi za Bayern Munich.

Jota anatarajiwa kushirikiana pakubwa na Roberto Firmino, Salah na sajili mpya Darwin Nunez katika safu ya mbele ya Liverpool baada ya Mane kuondoka.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Cesc Fabregas ajiunga na Como FC inayoshiriki Ligi ya Serie...

Mama ashauri korti imnyime mwanawe dhamana kwa sababu ya...

T L