• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Chelsea waangusha Palace ugani Stamford Bridge na kumpunguzia kocha Graham Potter presha ya kupigwa kalamu

Chelsea waangusha Palace ugani Stamford Bridge na kumpunguzia kocha Graham Potter presha ya kupigwa kalamu

Na MASHIRIKA

CHELSEA walimpunguzia kocha Graham Potter presha ya kutimuliwa baada ya bao la Kai Havertz kuwavunia ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ugani Stamford Bridge mnamo Jumapili.

Bao hilo la pekee lililofungwa na Havertz kwa kichwa, lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na mshambuliaji matata raia wa Morocco, Hakim Ziyech.

Matokeo hayo yalikomesha rekodi duni ya Chelsea waliokuwa wamepoteza mechi tatu mfululizo katika mashindano yote.

“Wiki chache zilizopita zimekuwa ngumu sana kwa Chelsea. Kila mmoja kambini amekuwa katika presha baada ya visa vingi vya majeraha kulemaza uthabiti wa kikosi,” akasema Havertz, 23.

Havertz ambaye ni raia wa Ujerumani, alipoteza nafasi murua za kufungia Chelsea bao la pili licha ya kupokezwa krosi nzuri na Mason Mount.

Palace nusura wasawazishiwe na Cheick Doucoure mwishoni mwa kipindi cha pili ila kombora lake likapanguliwa kwa ustadi mkubwa na kipa Kepa Arrizabalaga.

Matokeo hayo yalisaza Chelsea katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa jedwali la EPL kwa alama 28 sawa na nambari tisa Liverpool. Palace wanakamata nafasi ya 12 baada ya kupokezwa kichapo cha tano kutokana na mechi sita za mashindano yote.

MATOKEO YA EPL (Jumapili):

Chelsea 1-0 Palace

Newcastle 1-0 Fulham

Tottenham 0-2 Arsenal

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Rennes waangusha miamba PSG katika Ligi Kuu ya Ufaransa

Arsenal wapepea EPL

T L