• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 10:50 AM
Chelsea yazidisha ukatili

Chelsea yazidisha ukatili

LONDON, Uingereza

Na MASHIRIKA

Chelsea waliendeleza ubabe wao walipoandikisha ushindi wa 2-1 dhidi ya Watford Jumatano usiku na sasa wako juu ya jedwali kwa pointi 33 kutokana na mechi 14 mbale ya Manchester City walio na 32.

Mabao ya Mason Mount na Hakim Ziyech yalichangia ushindi huo baada ya mabingwa hao watetezi kutoka sare 1-1 na Manchester United, mwishoni mwa wiki.Licha ya ushindi huo, Chelsea ilipatwa na pigo kufuatia kuumia kwa Trevor Chalobah ambaye huenda asicheze mwishoni mwa wiki dhidi ya West Ham United.

Akizungumza baada ya mechi yao dhidi ya Watford, kocha Thomas Tuchel alitoa taarifa kuhusu jeraha la kinda huyo ambaye amekuwa msimu mzuri.“Tunarejea uwanjani Jumamosi, lakini jeraha la Trevor linanipa wasi wasi. Kuna wengine walioumia mbali na yeye.

Tulishuhudia daktari akiingia uwanja mara 20 kutibu wachezaji. Kukosekana kwa Trevor ni pigo kubwa kwa kikosi kizima, wakati huu tayari tunatarajia kuwakosa wachezaji kadhaa.”Mbali na Trevor, mastaa wengine wanaouguza majeraha ni Ben Chilwell, Reece James, Jorgihno, N’Golo Kante, Matteo Kovacic na Timo Werner.

Majeraha haya yametokea wakati Chelsea wakisubiri kurejea kwa Romelu Lukaku ambaye amekosa mechi sana kutokana na jeraha.Amekuwa akiingizwa katika kipindi cha pili kwenye mechi mbili za karibuni, lakini kiwango chake hakijarejea.

Tuchel ameeleza sababu ya kumuingiza Saul Niquez katika mechi hiyo iliyochezewa Vacarage Road ambayo ilisimamishwa kwa dakika kadhaa wakati shabiki alipokuwa akitibiwa baada ya kupatwa na ugonjwa wa moyo ghafla.

“Kutokana na majeraha kwa wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza, ilibidi nimwingize katika timu baada ya Trevor kuumia.’Kocha huyu amekiri kwamba kikosi chake kilikuwa na bahati ya kushinda mechi hiyo. “Kwa hakika hatukucheza vizuri.

Huenda sikupanga vyema kikosi changu. Hatukubalisha mchezo jinsi tulivyotarajia. Presha ilikuwa kubwa na tulifanya makosa mengi. Tutajaribu kurekebisha makosa hayo katika mechi ijayo dhidi ya west Ham United.

Kwingineko, FC Barcelona itachezea nje mechi zake za nyumbani kwa mwaka mmoja kutokana na ukarabati unaotarajiwa kufanyika kwenye uwanja huo.Klabu hii maarufu ina mpango wa miaka minne kuukarabati uwanja huo kwa ushirikiano na wafadhili wao.

Kulingana na mpango huo, ukarabati huo utamalizika rasmi mnamo 2025, mradi ambapo afisi za kisasa, hoteli na sehemu ya mazoezi zitajengwa.Barcelona wanatarajiwa kuchezea mechi zao uwanjani humo mwaka ujao kabla ya kuhamisha ratiba yao kwingoneko ukarabati huo utakaoanza.

You can share this post!

Onyango atawazwa bingwa wa ndondi

Kotut atawala mbio za Italia baada ya ukame wa miaka 3

T L