• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 7:50 AM
Eto’o asema ratiba ya AFCON haitabadilishwa

Eto’o asema ratiba ya AFCON haitabadilishwa

Na JOHN ASHIHUNDU

Kiongozi mpya wa Shirikisho la Soka Cameroon, Samuel Eto’o amesisitiza kwamba ratiba ya fainali za michuano ya kuwania ubingwa wa AFCON itafanyika kama ilivyopangwa.

Kumekuwa na maombi kutoka kwa timu husika zikitaka Chama cha Soka Afrika (CAF) kiahirishwe mechi hizo kufuatia kuibuka upya kwa Corona, pamoja pamoja na hatua ya klabu za Ulaya kukataa kuachilia wachezaji wao wajiunge na timu za mataifa hayo.

Lakini Eto’o ambaye ni jagina wa Afrika amefutilia mbali habari hizo, huku akithibitisha kwamba kila kitu kitafanyika kama ilivyopangwa. “Kwa nini yasifanyike? Eto’o aliwauliza wandishi wa habari za michezo. “Shirika ninalosimamia litatetea vikali mashindano haya.  Fainali za Euro zilifanyika wakati Corona ilikuwa imeenea kila mahali kote duniani huku mashabiki wakijazana viwanjani kushuhudia mechi hizo.

Kwa nini yetu isifanyike? Lazima tuelezane ukweli hapa.” Rwanda haikufuzu kwa fainali hizi, lakini raia wake Salma Radia Mukansanga ni miongoni mwa waamuzi wa kike watakaosimamia mechi hizo, baada ya jina lake kuwekwa kwenye orodha ya CAF ya waamuzi walioteuliwa.

Eto’o ambaye zamani alichezea klabu za Barcelona, Inter Milan na Chelsea alisema afisi yake itashirikisha wanasoka katika suala la kubuni sera zitakazoinua mchezo huo kuanzia mashinani. Alisema majukumu ya wanasoka waliosaafu ni kupigania maslahi ya wachezaji, huku akiahidi pia kujenga angalau viwanja 19 vipya vya klo,ataiofa nchiniCameroon.

Mshindi huyo mara nne wa taji la Mchezaji Bora Afrika mwenye umri wa miaka 40 alimshinda Seidou Mbombo Njoya katika uchaguzi uliofanyika majuzi nchini humo.

You can share this post!

Ruto apiga chenga Raila, Uhuru kuhusu mswada

Kesi ya ukwepaji ushuru dhidi ya Bilionea Kariuki...

T L