• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 10:55 PM
Kesi ya ukwepaji ushuru dhidi ya Bilionea Kariuki yasimamishwa

Kesi ya ukwepaji ushuru dhidi ya Bilionea Kariuki yasimamishwa

Na RICHARD MUNGUTI

MTENGENEZAJI pombe kali bilionea Humphrey Kariuki jana alipata afueni mahakama kuu ilipositisha kusikizwa kwa kesi inayomkabili ya kukwepa kulipa ushuru wa Sh17bilioni.

Jaji Antony Mrima alimwagiza hakimu mkuu Kagendo Michemi akome kusikiza kesi inayomkabili Bw Kariuki na washukiwa wengine saba hadi kesi iliyowasilishwa katika mahakama kuu isikizwe na kuamuliwa. Jaji Mrima alisema Bw Kariuki amehoji uhalali wa kesi inayomkabili akisema mamlaka ya ushuru nchini haipasi kuruhusiwa kuongoza kesi hiyo ilhali ndiyo iliichunguza.

Katika kesi aliyowasilisha katika mahakama kuu Bw Kariuki amesema haki zake zimekandamizwa kwa vile sheria za ushuru nchini zaipa KRA uwezo wa kuamua masuala yote kuhusu ushuru. Bw Kariuki ameilalamikia mahakama kuu kwamba kisheria maafisa wa polisi hawapasi kuingilia masuala ya ulipaji ushuru.

Jaji Mrima atasikiza kesi hiyo Feburuari 10,2022.

You can share this post!

Eto’o asema ratiba ya AFCON haitabadilishwa

Muturi awaita wabunge tena kujadili mswada tata wa vyama...

T L