• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 8:50 AM
Everton na Liverpool waumiza nyasi bure katika gozi la EPL ugani Goodison Park

Everton na Liverpool waumiza nyasi bure katika gozi la EPL ugani Goodison Park

Na MASHIRIKA

KOCHA Jurgen Klopp amekiri kuwa kusuasua kwa Liverpool “kumeanza kuzua hofu” baada ya makali yao kudidimia na miguu ya wavamizi wake kuingia kutu.

Miamba hao walioambulia nafasi ya pili ligini msimu jana baada ya kufukuzana na Manchester City hadi dakika za mwisho, sasa wametia kapuni alama tisa baada ya kushinda mechi mbili, kupiga sare tatu na kupoteza mara moja.

Pointi hizo ndizo chache zaidi kwa Liverpool kuwahi kujizolea kutokana na mechi sita za EPL chini ya Klopp aliyeanza kudhibiti mikoba yao mnamo Oktoba 2015. Japo wamefunga mabao 15 kufikia sasa, tisa yalitokana na mchuano mmoja – katika ushindi wa 9-0 dhidi ya Bournemouth mnamo Agosti 27 uwanjani Anfield.

Pambano la Septemba 7, 2022 dhidi ya Napoli ya Italia katika Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) ni mwanzo wa kibarua kigumu zaidi kwa Liverpool ambao licha ya kusajili Darwin Nunez, bado hawajafaulu kujaza kikamilifu pengo la Sadio Mane aliyeyoyomea Bayern Munich ya Ujerumani.

Baada ya kuendea Napoli, Klopp ataongoza masogora wake kumenyana na mbwa-mwitu Wolverhampton Wanderers ligini kabla ya kualika Ajax ya Uholanzi kwa ajili ya UEFA kisha kupepetana na Chelsea katika EPL ugani Stamford Bridge.

“Hii si Liverpool iliyofukuzia mataji manne kutoka mwanzo hadi mwisho wa muhula jana kabla ya kujinyanyulia Kombe la FA na ubingwa wa Carabao Cup hatimaye,” akasema fowadi wa zamani wa klabu hiyo, Peter Crouch.

“Hawachezi kwa kujituma licha ya kujivunia huduma za baadhi ya wanasoka wazoefu na bora zaidi duniani. Liverpool walikosea sana kumwachilia Mane kuondoka Anfield na watajuta,” akaongezea.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

  • Tags

You can share this post!

Montreal anayochezea Wanyama yang’ata Toronto MLS

MWALIMU WA WIKI: Mwangi ni mkuu si tu kwa maneno

T L