• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Montreal anayochezea Wanyama yang’ata Toronto MLS

Montreal anayochezea Wanyama yang’ata Toronto MLS

Na GEOFFREY ANENE

CF Montreal ilitoka chini mabao mawili na kunyamazisha wenyeji Toronto 4-0 kwenye Ligi Kuu ya Amerika na Canada (MLS) uwanjani BMO Field, Jumatatu.

Katika mchuano huo ambao kiungo Mkenya Victor Wanyama alicheza wote, Federico Bernardeschi alitetemesha nyavu za Montreal dakika ya tano kupitia penalti iliyosababishwa na Samuel Piette.

Lorenzo Insigne aliimarisha uongozi wa Toronto dakika mbili baadaye kupitia krosi ya Bernardeschi, lakini vijana wa kocha Wilfried Nancy ndio walifurahia kuenda mapumzikoni kifua mbele 3-2 baada ya Kamal Miller, Djordje Mihailovic na Kei Kamara kuona lango mara moja kila mmoja katika dakika ya 19, 21 na 43 mtawalia.

Alistair Johnston alipachika bao la nne la Montreal dakika 54 kabla ya Insigne kupata lake la pili zikisalia sekunde chache mechi ikatike.

Philadelphia Union wamekaa juu ya jedwali la Mashariki la MLS kwa pointi 60 kutokana na mechi 30. Philadelphia imejikatia tiketi ya mechi za muondoano.

Nambari mbili Montreal imezoa pointi 52 baada ya kujibwaga uwanjani mara 29. New York Red Bulls (alama 47), New York City (45), Orlando City (42), Columbus Crew (40) na New England Revolution (38).

Los Angeles FC wanaongoza kanda ya Magharibi, ambalo pia linajumuisha klabu 14, kwa pointi 60 wakifuatiwa na Austin (51), FC Dallas (46), Nashville (45), Minnesota (44), Real Salt Lake (42) na Portland (42). Timu saba za kwanza kutoka makundi hayo mawili zitaingia awamu ya muondoano.

  • Tags

You can share this post!

Ruto awanyooshea Uhuru na Raila mkono wa maridhiano

Everton na Liverpool waumiza nyasi bure katika gozi la EPL...

T L