• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Fainali za Elijah Lidonde kuchezwa Ijumaa ugani Bukhungu

Fainali za Elijah Lidonde kuchezwa Ijumaa ugani Bukhungu

NA JOHN ASHIHUNDU

MBIVU na mbichi kwenye makaka ya kwanza ya mashindano ya Elijah Lidonde kwa timu za vijana itajulikana Ijumaa mjini Kakamega wakati timu zitakutana kuwania mataji ya wasiozidi umri wa miaka 15 na wasiozidi umri wa miaka 17.

Mechi za nusu-fainali zinatarajiwa kufanyika Alhamisi katika uwanja wa Masinde Muliro University of Science and Technology (MMUST), ambapo washindi watasonga mbele kukutana ugani Bukhungu kwa fainali.

Mashindano hayo chini ya Wakfu wa Elijah Lidonde Foundation yalianzia katika ngazi ya Wadi za Kaunti ya Kakamega, huku timu 6,000 kutoka Wadi 60 zikishiriki.

Katika mahojiano ya mwenyekiti wa wakfu huo, Washington Muhanji, zamani kipa wa AFC Leopards na Harambee Stars, mbali na vikombe, washindi wataondoka na vocha za kununua bidhaa madukani, kwa vile sharia za FIFA haziruhusu vijana kupewa pesa kama zawadi.

Muhanji alisema waandalizi wameshuhudia vipaji vya hali ya juu tangu mashindano hayo yaanze miezi mitatu iliyopita chini ya ufadhili wa mlezi Alex Muteshi akishirikiana na Madiwani wa Wodi zote.

Mwenyekiti wa Elijah Lidonde Foundation Washington Muhanji (kushoto). PICHA | JOHN ASHIHUNDU

Alisema miongoni mwa wageni waliothibitisha kuhudhuria fainali za Ijumaa ni pamoja na Waziri mwenye Mamlaka Makubwa Musalia Mudavadi na Waziri wa Michezo.

AFC Leopards wanaoshikilia ubingwa wa timu za watu wakubwa, baada ya kuibwaga Nzoia Sugar 8-7 kupitia kwa mikwaju ya penalti, mwezi Oktoba 2022.

Mbali na Muhanji, wanasoka wengine wa zamani kwenye Wakfu hiyo ya Elijah Lidonde ni Alfred Imonje kama Katibu Mtendaji, Winna Shilavula (katibu), Anthony Okumu (mweka hazina), Fred Serenge, Nick Yakhama, Ngaira Esese na Tony Lidonde ambaye ni mwanaye marehemu Elijah Lidonde.

  • Tags

You can share this post!

Uhuru azuru Kaunti ya Mombasa kimyakimya

Ababu aomba CAF irejeshe Harambee Stars dimba la AFCON 2023

T L