• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Omanyala kutolewa jasho na Waamerika Kip Keino Classic

Omanyala kutolewa jasho na Waamerika Kip Keino Classic

Na AYUMBA AYODI

KIBARUA kigumu kinasubiri bingwa mtetezi Ferdinand Omanyala baada ya watimkaji matata Marvin Bracy, Kenney Bednarek, Aaron Brown, Jerome Blake na Arthur Cisse kujitosa Kip Keino Classic ugani Kasarani mnamo Mei 13.

Mwamerika Bracy ni mshindi wa nishani ya fedha katika mbio za mita 100 na 4x100m duniani.

Brown na Blake kutoka Canada ni mabingwa wa dunia wa 4x100m.

Mwamerika Bednarek alishinda medali ya fedha katika 200m kwenye Olimpiki 2020 na Riadha za Dunia 2022 naye Cisse anajivunia nishani ya fedha ya 100m kutoka michezo ya Afrika 2019.

“Mambo yanazidi kuwa mazuri Kip Keino Classic. Tuko tayari kwa makala haya ya nne ambapo vitengo tisa vitakavyowaniwa karibu vijazwe,” alisema msimamizi wa shindano hilo, Barnaba Korir.

Omanyala, ambaye ana muda bora kuliko wakimbiaji wote wa 100m (sekunde 9.77), na Bracy (9.85) walikutana katika nusu-fainali kwenye Riadha za Dunia jimboni Oregon, Amerika, Julai 2022.

Afisa wa polisi Omanyala alikamata nafasi ya tano kwa sekunde 10.14, akikosa kusonga mbele, huku Bracy akiingia fainali kwa kumaliza nambari mbili kwa 9.93.

Hata hivyo, Bracy aliridhika na fedha baada ya kuandikisha 9.88 dhidi ya Mwamerika mwenzake 9.86. Omanyala alikuwa amelemea Kerley walipoandikisha 9.85 na 9.92 katika Kip Keino Classic, mtawalia.

Bracy aliyemaliza nambari nane kwa 10.26 katika shindano la LSU Alumni Gold mnamo Aprili 23, alijiondoa kushiriki Botswana Golden Grand Prix Jumamosi iliyopita.

Omanyala aliwaonyesha kivumbi Bednarek, Brown na Blake katika Botswana Golden Grand Prix alipotimka 9.78.

Letsile Tebogo aliridhika na nafasi ya pili (9.91) akifuatiwa na Bednarek (10.02) na Brown (10.06) naye Blake akawa nambari nane (10.39).

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Sheria 400 hatarini kufuatia uamuzi wa wabunge

Faith Chepng’etich amezea mate 42km baada ya Sifan...

T L