• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 5:55 AM
Falcao arejea Uhispania kuchezea Rayo Vallecano baada ya kuondoka Galatasaray

Falcao arejea Uhispania kuchezea Rayo Vallecano baada ya kuondoka Galatasaray

Na MASHIRIKA

FOWADI Radamel Falcao wa Colombia amejiunga na kikosi cha Rayo Vallecano baada ya kuagana na Galatasaray.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 anarejea Uhispania kunogesha Ligi Kuu ya La Liga miaka minane tangu abanduke kambini mwa Atletico Madrid na kuyoyomea Ufaransa kuvalia jezi za AS Monaco.

Akiwa na Atletico, Falcao aliongoza kikosi hicho kunyanyua taji la Copa del Rey, Europa League na Uefa Super Cup.Alijiunga na Monaco mnamo 2013 na akawajibikia pia Manchester United na Chelsea kwa mkopo kati ya 2014 na 2016 kabla ya kutua Galatasaray waliompokeza mkataba wa kudumu mnamo 2019.

Falcao alifungia Galatasaray mabao 19 kwenye mechi 34 za Ligi Kuu ya Uturuki katika kipindi cha misimu miwili iliyomshuhudia akipata majeraha yaliyomweka nje kwa kipindi kirefu.

Kabla ya kuagana na Galatasaray, aliwajibishwa mara tatu pekee katika kampeni za msimu huu wa 2021-22.

  • Tags

You can share this post!

Ruto kukabiliwa na mtihani mkali 2022 akiepuka miungano

Ufaransa yateleza tena huku Uholanzi ikitamba katika mechi...