• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Fowadi Youssoufa Moukoko arefusha mkataba wake kambini mwa Borussia Dortmund hadi Juni 2026

Fowadi Youssoufa Moukoko arefusha mkataba wake kambini mwa Borussia Dortmund hadi Juni 2026

Na MASHIRIKA

MSHAMBULIAJI Youssoufa Moukoko amerefusha mkataba wake kambini mwa Borussia Dortmund hadi Juni 30, 2026.

Mkataba wa awali wa chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 ulitarajiwa kutamatika rasmi mwishoni mwa msimu huu wa 2022-23 na tayari alikuwa akimezewa mate na vikosi vya haiba kubwa barani Ulaya vikiwemo Chelsea na Barcelona.

Moukoko amekuwa tegemeo kubwa kambini mwa Dortmund tangu aagane rasmi na kikosi cha St Pauli mnamo 2016.

“Ingawa ni fahari tele kuwaniwa na klabu kadhaa maarufu, nimehiari kusalia kambini mwa Dortmund, na huo ndio uamuzi kutoka moyoni mwangu,” akasema Moukoko.

Moukoko alikuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani katika fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar na alitokea benchi dhidi ya Japan katika mojawapo ya mechi za makundi.

Amefungia Dortmund mabao sita na kuchangia sita mengine kutokana na mechi 22 kufikia sasa msimu huu.

“Moukoko ni mchezaji wa haiba kubwa ambaye tumemlea kambini mwa Dortmund. Ametuonyesha ukubwa wa uwezo wake uwanjani na bado ana fursa ya kuimarika zaidi ulingoni,” akasema mkurugenzi wa soka kambini mwa Dortmund, Sebastian Kehl.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kocha Frank Lampard katika hatari ya kutimuliwa ugani...

Kipkirui na Cheserek watamba Santa Pola Half Marathon...

T L