• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 5:55 AM
Gor Mahia kujua mpinzani wao kwenye mchujo wa Kombe la Mashirikisho barani Afrika

Gor Mahia kujua mpinzani wao kwenye mchujo wa Kombe la Mashirikisho barani Afrika

Na CHRIS ADUNGO

MABINGWA wa soka ya humu nchini, Gor Mahia watafahamu leo Ijumaa atakayekuwa mpinzani wao kwenye mchujo wa kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Mashirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup) msimu huu wa 2020-21.

Droo ya mapambano hayo yatakayoleta pamoja washindi 16 wa raundi ya kwanza ya hatua ya 32-bora kwenye Confederation Cup na vikosi 16 vilivyoaga mchujo wa raundi 32-bora ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League) itafanyika leo jijini Cairo, Misri.

Pia kutafanywa droo ya hatua ya makundi ya kampeni za CAF Champions League, mapambano ambayo Gor Mahia waliaga baada ya kudenguliwa kwa jumla ya mabao 8-1 kutoka kwa CR Belouizdad ya Algeria.

Mechi za mkondo wa kwanza kwenye mchujo wa Confederation Cup zitasakatwa mnamo Februari 14 kabla ya marudiano kuandaliwa wiki moja baadaye. Washindi wa mechi hizo za mikondo miwili watafuzu kwa droo ya hatua ya makundi itakayofanyika Februari 22.

Gor Mahia watakuwa wenyeji wa mkondo wa kwanza wa mchujo huo na wakutanishwa na mojawapo ya timu zilizofuzu kwa hatua ya 16-bora ya Confederation Cup.

Kati ya klabu hizo ni Entente Setif, JS Kabylie (zote za Algeria), Etoile Sahel, US Monastir (zote za Tunisia), Renaissance Berkane (mabingwa watetezi kutoka Morocco), Tihad Casablanca (Morocco), Coton Sport (Cameroon), DC Motema Pembe (DR Congo), Jaraaf (Senegal), AS Kigali (Rwanda), Namungo (Tanzania), NAPSA Stars (Zambia), Orlando Pirates (Afrika Kusini), Pyramids (Misri), Salitas (Burundi) na mshindi kati ya Rivers Utd (Nigeria) na Bloemfontein Celtic (Afrika Kusini).

Mbali na Gor Mahia, vikosi vingine vilivyoaga hatua ya 32-bora ya CAF Champions League na ambavyo vitakuwa wenyeji wa mkondo wa kwanza wa mchujo wa Confederation Cup ni Al Ahly Benghazi (Libya), Bouenguidi (Gabon), CS Sfaxien (Tunisia), Enyimba (Nigeria), Gazelle (Chad), Jwaneng Galaxy (Botswana), Nkana (Zambia), Platinum (Zimbabwe), Primeiro Agosto (Angola), Racing Club Abidjan (Ivory Coast), Raja Casablanca (Morocco), Sonidep (Niger), Stade Malien (Mali), Young Buffaloes (Swaziland) na mshindi kati ya Al Hilal (Sudan) na Asante Kotoko (Ghana).

Mechi za hatua ya makundi kwenye CAF Champions League zimeratibiwa kupigwa kati ya Februari 12-13, Februari 23, Machi 5-6, Machi 16, Aprili 2-3 na Aprili 9-10. Washindi wawili wa kwanza katika kila kundi watafuzu kwa droo ya robo-fainali itakayofanyika Aprili 30.

WASHINDI 16-BORA WA CAF CHAMPIONS LEAGUE:

Al Ahly, Zamalek, CR Belouizdad, Mouloudia Alger, Chiefs, Mamelodi Sundowns, TP Mazembe, V Club, Al Merrikh, Esperance, Horoya, Petro Luanda, Simba, Teungueth, Wydad Casablanca na mshindi kati ya Al Hilal na Asante Kotoko.

WASHINDI 16-BORA WA CAF CONFEDERATION CUP:

Entente Setif, JS Kabylie, Etoile Sahel, US Monastir, Renaissance Berkane, Tihad Casablanca, Coton Sport, DC Motema Pembe, Jaraaf, AS Kigali, Namungo, NAPSA Stars, Orlando Pirates, Pyramids, Salitas na mshindi kati ya Rivers Utd na Bloemfontein Celtic.

VIKOSI 16 VILIVYOAGA HATUA YA 32-BORA YA CAF CHAMPIONS LEAGUE:

Gor Mahia, Al Ahly Benghazi, Bouenguidi, CS Sfaxien, Enyimba, Gazelle, Jwaneng Galaxy, Nkana, Platinum, Primeiro Agosto, Racing Club Abidjan, Raja Casablanca, Sonidep, Stade Malien, Young Buffaloes na mshindi kati ya Al Hilal na Asante Kotoko.

You can share this post!

BBI kuangushwa katika kura ya maamuzi – Utafiti

Mamia ya wakazi wakosa nafasi za wana wao katika shule za...