• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Haaland atambisha Man-City dhidi ya Borussia Dortmund katika pambano la UEFA ugani Etihad

Haaland atambisha Man-City dhidi ya Borussia Dortmund katika pambano la UEFA ugani Etihad

Na MASHIRIKA

FOWADI Erling Haaland aliongoza Manchester City kutoka nyuma na kuzamisha chombo cha Borussia Dortmund 2-1 katika mchuano wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Jumatano usiku ugani Etihad.

Dortmund waliwekwa kifua mbele na Jude Bellingham aliyeshirikiana vilivyo na nahodha Marco Reus katika dakika ya 56.

Hata hivyo, masogora wa kocha Pep Guardiola walisawazishiwa na John Stones katika dakika ya 80 kabla ya Haaland kumwacha hoi kipa Alexander Meyer dakika nne kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa kipindi cha pili kupulizwa. Bao la Haaland ambaye ni raia wa Norway, lilikuwa zao la ushirikiano wake na Joao Cancelo.

Ilikuwa mechi ya kwanza kwa sogora huyo wa zamani wa RB Salzburg ya Austria kutandaza dhidi ya Dortmund waliomwachilia ajiunga na Man-City muhula huu.

Bao la Haaland lilikuwa lake la 13 msimu huu na la 26 kutokana na mechi 21 za UEFA.

Man-City sasa wanaselelea kileleni mwa Kundi G kwa alama sita baada ya kufungua kampeni za UEFA msimu huu kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Sevilla mnamo Septemba 6, 2022. Dortmund ni wa pili kundini kwa alama tatu, mbili zaidi kuliko FC Copenhagen ya Denmark na Sevilla ya Uhispania.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Real Madrid wapepeta RB Leipzig ya Ujerumani katika gozi la...

NGUVU ZA HOJA: Chuo Kikuu cha Baraton ni mfano wa kuigwa na...

T L