• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Harry Kane afikia rekodi ya Sergio Aguero kwa kunyanyua taji la Mchezaji Bora wa Mwezi wa EPL

Harry Kane afikia rekodi ya Sergio Aguero kwa kunyanyua taji la Mchezaji Bora wa Mwezi wa EPL

Na MASHIRIKA

FOWADI wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, ametawazwa Mchezaji Bora wa Mwezi katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa mara ya saba na hivyo kufikia rekodi iliyowahi kuwekwa na aliyekuwa mshambuliaji matata wa Manchester City, Sergio Aguero.

Kane, 28, alipachika wavuni mabao manne na kuchangia mawili mengine mnamo Machi 2022 na hivyo kusaidia waajiri wake kuweka hai matumaini ya kukamilisha kampeni za EPL ndani ya mduara wa nne-bora msimu huu na hivyo kufuzu kwa kipute cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo 2022-23.

Aguero aliyestaafu soka mnamo Disemba 2021, alizoa taji la Mchezaji Bora wa Mwezi katika EPL kwa mara ya mwisho mnamo Januari 2020. Fowadi na nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard anasoma migongo ya Kane na Aguero baada ya kuzoa taji hilo mara sita.

Tuzo hiyo ambayo imekuwa ikitolewa tangu 1994, ilitwaliwa kwa mara ya kwanza na mshambuliaji wa zamani wa Tottenham, Jurgen Klinsmann. Mnamo Februari 2022, Kane alivunja rekodi ya Wayne Rooney aliyewahi kufunga mabao mengi zaidi katika EPL. Alifunga bao lake la 95 katika mechi hiyo iliyowashuhudia wakizamisha Brighton 2-0.

Mkufunzi Mikel Arteta wa Arsenal alishinda taji la Kocha Bora wa Mwezi Machi katika EPL baada ya kuongoza waajiri wake kutinga orodha ya nne-bora ligni baada ya kushinda mechi tatu kati ya nne.

You can share this post!

Kalonzo apanga UhuRaila

KOMBE LA DUNIA: Kibarua kizito kwa vikosi vya Afrika nchini...

T L