• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 11:13 AM
Kalonzo apanga UhuRaila

Kalonzo apanga UhuRaila

ELVIS ONDIEKI na LEONARD ONYANGO

KINARA wa Wiper, Kalonzo Musyoka amefanikiwa kuwashinikiza Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM, Raila Odinga kubadili jina la muungano wa Azimio la Umoja.

Muungano huo sasa utajulikana kama Chama cha Azimio la Umoja-One Kenya.

Awali, viongozi wa ODM walikuwa wamepinga vikali pendekezo la Bw Musyoka kutaka muunganano huo utakaotumiwa na Bw Odinga kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, ubadilishe jina.

Bw Musyoka pia alitaka nembo ya muungano huo unaojumuisha vyama 24, ibadilishwe. Muungano huo umekuwa ukitumia herufi ‘R’ kumaanisha ‘Raila’ kama nembo yake.

Kinara huyo wa Wiper pia alitaka kutengewa asilimia 30 ya nyadhifa serikalini iwapo atakosa kuteuliwa kuwa mwaniaji mwenza wa Bw Odinga.

Tangu Bw Musyoka kutangaza kujiunga na Azimio mwezi uliopita, hajakuwa akifanya kampeni pamoja na Bw Odinga.

Jana, Katibu Mkuu wa Kanu Nick Salat alisema viongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya wataanza mkutano wa kwanza wa pamoja leo katika Kaunti ya Pokot Magharibi na kisha kuelekea Kaunti ya Turkana kesho.

Katika taarifa ya pamoja iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Wiper, Shakila Abdalla ambaye pia ni Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Lamu, makatibu hao walisema miongoni mwa stakabadhi zilizotiwa saini ni barua rasmi ya kuomba Msajili wa Vyama vya Kisiasa Ann Nderitu kusajili muungano huo.

Alisema makatibu hao pia walitia saini ya mkataba wa maelewano kutambua Bw Odinga kuwa mwaniaji wa urais wa muungano wa Azimio la Umoja-Kenya Kwanza. “Vyama vyote vilivyo ndani ya muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya vinatambua Bw Odinga kama mwaniaji wa urais,” akasema Bi Abdalla.

Alisema Bw Musyoka sasa ataongoza kampeni za Bw Odinga japo bado haijulikani ikiwa kinara wa ODM alikubali kumtengea asilimia 30 ya nyadhifa serikalini au kumteua kuwa mwaniaji mwenza.

“Kuanzia kesho (leo) viongozi wetu wataanza kufanya kampeni pamoja na watazuru maeneo yote nchini. Hiyo itakuwa ishara kwamba tumekubali kushirikiana ili tuunde serikali ijayo,” akasema Seneta wa Kitui, Enoch Wambua.

Bw Musyoka ndiye mwasisi wa muungano wa One Kenya Alliance (OKA).

Bw Javas Bigambo, mdadisi wa masuala ya kisiasa anasema kuwa Bw Musyoka huenda alitaka jina la muungano wake wa OKA kujumuishwa ili atambuliwe kama mmoja wa vinara wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya.

“Iwapo jina la muungano huo lingesalia Azimio la Umoja, Kalonzo angemezwa na kusahaulika. Jina hilo jipya limempa usemi ndani ya muungano kama mmoja wa vinara.

  • Tags

You can share this post!

Safari ya Arsenal kwenye UEFA msimu huu yakatizwa na vipusa...

Harry Kane afikia rekodi ya Sergio Aguero kwa kunyanyua...

T L