• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 7:50 AM
Janet Okello: Kenya Lionesses ina kibarua kigumu kuingia Olimpiki

Janet Okello: Kenya Lionesses ina kibarua kigumu kuingia Olimpiki

Na GEOFFREY ANENE

NYOTO Janet ‘Shebesh’ Okello amebashiri Ijumaa kuwa wapinzani wakuu wa Kenya Lionesses kwenye Kombe la Afrika la raga ya wachezaji sana kila upande watakuwa Afrika Kusini na Madagascar.

Kombe hilo litafanyika Oktoba 14-15 jijini Tunis nchini Tunisia ambako Kenya itawania ubingwa wa Afrika na tiketi ya kuingia Olimpiki 2024 dhidi ya Afrika Kusini, Tunisia, Zimbabwe, Uganda, Madagascar, Zambia na Ghana.

Droo ya dimba hilo la mataifa manane ilifanywa Julai 19, huku Kenya ya kocha Dennis Mwanja ikitiwa Kundi B pamoja na Madagascar, Zambia na Ghana. Kundi A linajumuisha mabingwa watetezi Afrika Kusini pamoja na Tunisia, Uganda na Zimbabwe.

Afrika Kusini ilichapa Madagascar 15-14 katika fainali mwaka 2022 nchini Tunisia.

Kenya iliyokuwa imefika fainali ya kombe hilo mwaka 2012, 2013, 2014, 2015, 2016, 2017 na 2019 na kushinda 2018, haikuwa na lake 2022 iliporidhika na nafasi ya tano.

Wakenya walishiriki Olimpiki mwaka 2016 nchini Brazil na 2020 nchini Japan baada ya kutunukiwa tiketi Afrika Kusini ilipojiondoa.

“Haitakuwa rahisi kwa sababu raga ya Afrika ya wanawake imeimarika sana. Lazima tufanye kazi kubwa ili kupata mafanikio. Tishio kubwa kwetu labda litatoka kwa Afrika Kusini na Madagascar,” alikiri Shebesh alipoulizwa na Taifa Leo kuhusu mashindano hayo na nafasi ya Kenya kuingia Olimpiki 2024 itakayofanyika jijini Paris, Ufaransa.

Shebesh ni mmoja wa nyota wa timu ya Kenya. Anacheza raga ya malipo katika klabu ya MIE Pearls nchini Japan.

  • Tags

You can share this post!

Soko jipya la Makongeni mjini Thika kugharimu Sh400 milioni

Sabina asema Uhuru anafaa kumshukuru badala ya kumlaumu

T L