• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
KCB yasaini wachezaji watano zaidi kwa ajili ya Ligi Kuu

KCB yasaini wachezaji watano zaidi kwa ajili ya Ligi Kuu

NA GEOFFREY ANENE

WANABENKI wa KCB FC wamekamilisha shughuli ya kuimarisha kikosi baada ya kusajili wachezaji watano wapya huku Kamati ya Mpito ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF) ikiongeza muda wa kufanya usajili hadi Septemba 7.

Wachezaji wapya ni Hillary Ojiambo kutoka Soy United, Bramwell Kipkorir (Society 43 Nakuru), Edmond Erick (Gogo Boys FC), Kennedy Owino (Wazito FC) na Haniff Wesonga kutoka shule ya upili.

Wanaungana na wachezaji nyota waliosajiliwa mapema soko lilipofunguliwa Nicholas Kipkirui, Francis Kairo, Harun Mwale, Kevin Otieno, Danson Chetambe na Byrne Omondi.

Wachezaji wapya wameelezea matumaini yao ya kupata fursa ya kuonyesha talanta zao mara ligi itakapoanza baadaye Septemba.

Mshambulizi Kairo, ambaye alifungia FC Talanta mabao tisa kwenye Ligi Kuu msimu 2021-2022, tayari ameridhisha kocha Zedekiah ‘Zico’ Otieno kwa kufunga mabao matatu katika michuano mitatu ya kirafiki ambayo KCB imesakata.

KCB watarejea uwanjani kupimana nguvu na Gor Mahia hapo Septemba 3 ugani ABSA mtaani Ruaraka.

  • Tags

You can share this post!

GUMZO LA SPOTI: Mtangoja sana, Viera aambia Arsenal na...

Conte: Ni wakati wa Kane kuongeza kandarasi yake

T L