• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 9:11 AM
Kenya Morans kuingia kambini Januari 11 kwa mechi za kufuzu AfroBasket

Kenya Morans kuingia kambini Januari 11 kwa mechi za kufuzu AfroBasket

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya Kenya Morans itaripoti kambini Januari 11 kujiandaa kwa duru ya kufa-kupona ya kuingia Kombe la Afrika la mpira wa vikapu la wanaume (AfroBasket) itakayoandaliwa Februari 19-21, 2021.

Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Vikapu Kenya (KBF) walikutana Januari 9 na kuamua tarehe hiyo na kuongeza kuwa Morans itafanyiwa vipimo vya kwanza vya virusi vya corona mnamo Januari 13 kabla ya kuzamia maandalizi Januari 15 uwanjani Nyayo.

Morans, ambayo ilivuna medali ya fedha kwenye Kombe la Afrika la wachezaji wanaocheza barani Afrika (AfroCan) mwaka 2019, itapimwa virusi hivyo mara tatu kabla ya kurudiana na Senegal, Angola na Msumbiji katika mechi za Kundi B.

Timu hizi zilimenyana katika duru ya kwanza Novemba 2020 ambapo Morans ilipoteza dhidi ya Senegal na Angola na kubwaga Msumbiji.

Wachezaji 10 wanaocheza mpira wa vikapu humu nchini watakuwa katika kundi la kwanza litakaloanza mazoezi. Wachezaji hao wanatarajiwa kutoka kikosi kilichochaguliwa kwa majukumu ya duru ya kwanza, ingawa kocha Cliff Owuor yuko huru kufanya mabadiliko.

Aidha, Kaimu Katibu wa KBF Ambrose Kisoi alieleza Taifa Leo kuwa serikali italeleza shirikisho hilo msimamo wa mwisho kuhusu bajeti ya Sh13 milioni juma hili.

Katika mahojiano ya awali, Kisoi alisema KBF imetuma ombi kwa Shirikisho la Mpira wa Vikapu Afrika (FIBA Africa) kutaka haki za kuwa mwenyeji wa duru hiyo ya mwisho ya Kundi B pamoja na kundi moja jingine.

Timu tatu za kwanza kutoka kila kundi zitafuzu kushiriki AfroBasket nchini Rwanda mwezi Agosti/Septemba 2021. Kenya haijakuwa kwenye AfroBasket tangu iandae fainali za 1993

  • Tags

You can share this post!

Borussia Monchengladbach watoka nyuma na kuzamisha chombo...

Malala amtaka Rais kuadhibu wanaomsumbua chamani