• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 2:00 PM
Kiatu cha dhahabu KWPL chapata ushindani mkali

Kiatu cha dhahabu KWPL chapata ushindani mkali

NA AREGE RUTH

BAADA ya raundi ya tisa ya michuano ya Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL), ushindani mkali unaendela kushuhudiwa upande wa ufungaji magoli.

Mshambuliaji wa Thika Queens Wendy Atieno, anaongoza kwenye orodha ya wafungaji bora akiwa na mabao 10 kufikia sasa.

Katika mechi za awali tatu, Atieno amefunga mabao matatu ‘Hattrick’ kwa mpigo. Alichangia ushindi wa (4-1) dhidi ya Kisumu All Starlets, akafunga dhidi ya Vihiga Queens ambapo walipata ushindi wa (4-1).Lakini  kwenye mechi hiyo, aliwapa Vihiga zawadi kwa kujifunga bao.

Pia, alicheka na wavu katika ushindi wa (5-1) dhidi ya Gaspo Women.

Chris Kach ambaye pia anasakatia Thika, ni wa pili bora akiwa na mabao saba nae mshambuliaji wa Kisumu All Starlets Monicah Etot, anafunga tatu bora akiwa na mabao sawa.

Lydia Akoth wa Gaspo Women ni wa nne bora na mabao sita, sawa na Maureen Ater (Vihiga) na Puren Alukwe wa (Zetech Sparks) ambao wameshikilia nafasi ya tano na sita mtawalia kwenye jedwali.

Kando na hayo, Kangemi Ladies ndiyo timu ambayo imefungwa mabao mengi zaidi ligini kufikia sasa. Mwezi Disemba 2022, walinyeshewa 12-0 na Vihiga katika mechi ya raundi tatu ya ligi. Kwa sasa timu hiyo imefungwa jumla ya mabao 42 na kuifanya kuwa timu ambayo imefungwa mabao mengi msimu huu.

Kangemi kwa sasa imeshikilia nafasi ya 11 kwenye jedwali na alama tatu. Alama hizo tatu walipata bila kutolea jasho dhidi ya Kayole Ladies ambao walisusia kucheza mechi hiyo.

Kayole ambao wako mkiani kwenye jedwali, wamefungwa jumla ya magoli 36. Sawa na Kangemi, pia walifungwa 11-0 na Gaspo Women mapema mwezi huu.

Kufikia sasa, wamepoteza mechi zote tisa za ligi na wanachungulia kushuka daraja ikiwa hawatashinda mechi zilisosalia za ligi.

Kwingineko, Mechi kati ya Kangemi na Trans Nzoia Falcons ambayo ilipangwa kuchezwa leo katika uwanja wa Ndura mjini Kitale, imehairishwa hadi Ijumaa wiki hii.

  • Tags

You can share this post!

Ruto atangaza rasmi kiti cha Chebukati kuwa wazi

Presnel Kimpembe aomba mashabiki msamaha baada ya kikosi...

T L