• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Kipusa Alexia Putellas wa Barcelona atawazwa mshindi wa Ballon d’Or

Kipusa Alexia Putellas wa Barcelona atawazwa mshindi wa Ballon d’Or

Na MASHIRIKA

NAHODHA wa Barcelona, Alexia Putellas, ndiye mshindi wa taji la Mchezaji Bora Duniani la Ballon d’Or kwa upande wa wanawake mnamo 2021.

Putellas, 27, alifunga bao na kusaidia Barcelona kupepeta Chelsea 4-0 na kuibuka mabingwa wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Alikamilisha kampeni za msimu wa 2020-21 akiongoza orodha ya wafungaji bora barani Ulaya baada ya kupachika wavuni mabao 26 katika mashindano yote na kutawazwa Mchezaji Bora na Kiungo Bora wa Uefa.

Putellas alibwaga mchezaji mwenzake kambini mwa Barcelona, Jennifer Hermoso na fowadi wa Chelsea, Sam Kerr walioambulia nafasi za pili na tatu mtawalia.

Mshambuliaji wa Arsenal, Vivianne Miedema, aliridhika na nafasi ya nne huku wanasoka watatu wa Chelsea – Pernille Harder, Jessie Fleming na Fran Kirby wakikamata nafasi za saba, tisa na 10 mtawalia.

Orodha ya washindi wa Ballon d’Or kwa wanawake:

1. Alexia Putellas (Barcelona / Uhispania, kiungo)

2. Jennifer Hermoso (Barcelona / Uhispania, fowadi)

3. Sam Kerr (Chelsea / Australia, fowadi)

4. Vivianne Miedema (Arsenal / Uholanzi, fowadi)

5. Lieke Martens (Barcelona / Uholanzi, kiungo)

6. Christine Sinclair (Portland Thorns / Canada, fowadi)

7. Pernille Harder (Chelsea / Denmark, kiungo)

8. Ashley Lawrence (Paris St-Germain / Canada, beki)

9. Jessie Fleming (Chelsea / Canada, kiungo)

10. Fran Kirby (Chelsea / Uingereza, fowadi)

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Donnarumma atawazwa Kipa Bora Duniani

Uhuru asema Raila na Mudavadi ndio walimjulisha bungeni

T L