• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 2:33 PM
Kocha wa Ingwe atarajiwa kuwasili Ijumaa

Kocha wa Ingwe atarajiwa kuwasili Ijumaa

BY JOHN ASHIHUNDU

Kocha wa AFC Leopards, Patrick Aussems anatarajiwa kurejea nchini leo kuendelea kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao utakaoanza wikendi ijayo.

Mbelgiji huyo mwenye umria wa 56 alitia saini mkataba mpya wa miaka miwili kabla ya kuondoka nchini mwezi uliopita, akimuachia Tom Juma mamlaka ya kunoa kikosi chini ushauri wake kupitia kwa mtandao.

Kupitia kwa ujumbe mtandaaoni, Aussems alihakikishia mashabiki juzi kwamba atarejea nchini kutekeleza wajibu wake. Kuondoka kwake gahfal kulikuwa kumezusha wasiwasi miongoni mwa mashabiki wa Ingwe.

Hii ni baada ya hapo awali timu nyingi nchini kushuhudia makocha wao wakitoweka mara wanapopewa ruhusa ya kwenda likizoni kwa shughuli za binafsi.

Lakini akizungmza jana, Juma alithibitisha kwamba amekuwa akiwasiliana na kocha huyo kila wakati huku wakibandilishana mawazo kuhusu mazoezi.

“Aussems amekuwa akifuatilia timu kwa karibu na tunamtarajia nchini kesho, siku ambayo tumepangiwa mechi ya kirafiki dhidi ya Modern Coast Rangers ya Mombasa wakati huu tunajiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21,” alisema kiungo huyo mstaafu wa kimataifa maarufu kama Gaza.

Tom alisema idara yake imegundua vijana kadhaa ambao watapewa nafasi wakati wa mechi ya kesho ugani Camp Toyoyo kuanzia saa sita mchana.

“Wachezaji wote wamerejea mazoezini isipokuwa Bienvenue Shaka pamoja na wachezaji wengine saba- Collins Shichenje, Clyde Senaji, Elvis Rubia, John Oyemba, Benjamin Ochan, Hansel Ochieng na Harrison Mwendwa,” aliongeza.

Alisema kocha amemshauri atafute walinzi wawili viungo mawili na washambuliaji wawili na washambuliaji wawili wasajiliwe wakati huu wa dirisha la uhamiaji nchini. Hata hivyo, itabidi Leopards isubiri kibali cha kusajili wachezaji wapya baada ya kupigwa marufuku na Fifa.

Leoipards imepigwa marufuku kusajili wachezaji wapya baada ya kushindwa kulipa wachezaji na makocha wao wa zamani, lakini Juma alisisitiza jana kwamba ako na wachezaji 20 ambao wanaweza kuendelea kushindania taji la ligi msimu ujao, licha ya hali ngumu ya kifedha.

  • Tags

You can share this post!

Kijana aunda Sh150,000 kutokana na magurudumu

Madereva Wahome, Hamza na Kimathi kupeperusha bendera ya...