• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 3:09 PM
Kocha wa Sugar RFC hofu vifaa tegemeo kukosekana ufunguzi wa Kenya Cup

Kocha wa Sugar RFC hofu vifaa tegemeo kukosekana ufunguzi wa Kenya Cup

Na TITUS MAERO

Mkufunzi mkuu wa Kabras Sugar RFC Jerome Muller, ameeleza wasiwasi wake kuwa wachezaji wake 12 hawatakuwepo kikosi chake kitakapocheza mechi yake ya ufunguzi katika Ligi Kuu ya Raga nchini (Kenya Cup), jumamosi hii.

Muller alisema kuwa wachezaji hao wake wako na timu ya taifa almaarufu Kenya Simbas (15s) ambayo iko nchini Afrika Kusini, na mchezaji mmoja yuko na timu ya taifa ya Shujaa (7s) ambayo iko Dubai.Timu ya Kenya Simbas inashiriki kwenye kivumbi cha Stellenbosch Challenge Trophy nchini Afrika Kusini na kinatamatika leo, ilhali Shujaa inashiriki kwenye kivumbii cha Dubai Sevens.

Kabras Sugar inafungua msimu wa 2021/2022 dhidi ya Blak Blad ya Chuo Kikuu cha Nairobi (UON) mjini Kakamega, kuanzia saa tisa.?Mchuano huo utaandaliwa katika uwanja wa Maonyesho ya kilimo ya Kakamega.?Kabras Sugar wamewahi shinda taji la Ligi Kuu mwaka wa 2016 wakiwa chini ya kocha Mike Bishop ambaye alikuwa raia wa nchi ya Australia.

Jana, Muller alitaja masogora wake ambao wako nchini Afrika Kusini kuwa Brian Tanga, Brian Juma, George Nyambua na Jone Kubu.?Wengine ni Epraim Odour, Joseph Odero, Dan Sikuta, Stephen Sakari, Barry Robinson, Eugene Sifuna na Derrick Ashiundu.

Naye, Kevin Wekesa yuko na Shujaa (7s) ambayo inashiriki kwenye mashindano ya Dubai Sevens.?Katika mahojiano na Taifa Leo mjini Kakamega jana, Muller alisema atachezesha wachezaji wake ambao wako na umahiri kidogo wa kucheza kiwango cha Ligi Kuu.

‘Nina masogora ambao wako na ustani kibao wa kusakata raga na niko na imani watatuwakilisha vyema,’ aliongeza.?Kwingineko, katika Ligi Kuu ya Raga (Kenya Cup) ya Kinadada, mechi nne zitasakatwa jumamosi hii jijini Nairobi.

Mwamba itapepetana na Too Fry Nakuru uwanjani RFUEA, huku Ruckit ikipambana na Yamananshi Impala katika uwanja wa Impala Club, Nairobi.?Vipusa wa Homeboyz watamenyana na Surburbs ugani Ruaraka, Nairobi.

You can share this post!

Matano roho juu CS Sfaxien ikiwasili, Gor ziarani Congo

Afueni Rudisha akifanyiwa upasuaji na kutangaza atarejea...

T L